Kurasa

Ijumaa, 22 Agosti 2014

BILA MILION 20 DIAMOND HAFANYI SHOW

Tangu mwaka juzi tulifahamu kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii wa Tanzania anaelipwa kiasi kikubwa cha pesa, na mwaka jana ikaelezwa kuwa bila milioni 10 au 8 za Kitanzania humpati kwenye show yako.
Lakini kiwango kipya kilichotajwa jana kitawapa kizunguzungu zaidi hasa mapromota wenye mitaji midogo wenye ndoto za kufanya kazi na mwimbaji huyo.
Kwa mujibu wa, Babu Tale ambaye ni meneja wake, hivi sasa kiwango cha chini anachochaji kwa show moja hapa nchini ni $15,000 (sawa na shilingi Milioni 25 za Tanzania).
“Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola e15,000.”Babu Tale aliiambia Bongo5.
Kwa mujibu wa Babu Tale, wanachaji kiasi cha hadi dola 25,000 kwa show moja za nje ya nchi (ikiwemo Marekani).
“Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya.”Alisema wakati akikanusha tuhuma kuwa Diamond anauza dawa za kulevya.
Kwa mahesabu ya haraka haraka, shows 15 mara dola 25,000 ni sawa na $375,000 (Sawa na shilingi za Tanzania 625,687,500).
Yesss! Ni zaidi ya Milioni mia sita ishirini na tano za kitanzania. Kama ni kweli, basi Diamond anastahili kweli kuitwa Dangote wa Bongo Flava.
Bado michongo inaendelea kumiminika ambapo hivi karibuni meneja wa Trey Songz alimtumia ujumbe kuwa atakapokuwa na nafasi amshitue waongee.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni