Kurasa

Jumatatu, 7 Julai 2014

UJASIRIAMALI UNA BADIRISHA MAISHA

UJASIRIAMALI una maana pana, miongoni mwa hizo ni kuwa na hamasa kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika uchumi.
Pia katika hali nyingine mjasiriamali anaweza kuwa mtu yeyote anayejishughulisha katika sekta fulani, mfano kilimo, ufugaji au biashara.
bonyeza hapa kusoma zaidi..



Kwa mitazamo mbalimbali ya wasomi, mjasiriamali ni mtu anayeongoza, anayepanga na aliye na utayari juu ya hatari zozote zinazoweza kujitokeza katika biashara husika.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa Ismail Lankii, aliyekuwa dalali wa pumba za mahindi na baadaye kuwa mjasiriamali anayesafirisha bidhaa hiyo kwenda kuuza nchini Kenya.
Katika mahojiano na Tanzania Daima, akielezea safari yake ya kuwa mjasiriamali, Lankii anasema mwaka 2009 kabla ya kujiari na kuanzisha biashara ya kununua pumba kutoka sehemu mbalimbali nchini alikuwa dalali wa shughuli hizo.
Lankii anasema udalali alioufanya ulikuwa wa biashara hiyo ya pumba, kazi aliyopewa na raia waliotoka Kenya waliokuja nchini kwa ajili ya kufanya biashara hiyo.
“Nilifanya shughuli ya udalali kwa uaminifu mkubwa huku nikiwa na ndoto ya kufanya biashara hiyo, mwaka 2009 niliachana na udalali na kuanza biashara yangu kwa mtaji kidogo,” anasema.
Anasema baada ya kuona biashara ya kununua pumba na kukausha kisha kusafirisha ina faida, aliomba mkopo wa sh milioni 15 Benki ya Taifa ya Biashara (NMB) ili kukuza mtaji wa biashara yake.
Mjasiriamali huyo anasema alipofanikiwa kupata mkopo NMB, alimshirikisha mkewe na kuafikiana kuwaajiri wafanyakazi watatu ili waweze kufanya biashara vizuri.
Anasema baada ya kupata mkopo, fedha hizo zilizalisha mtaji mkubwa na kufanikiwa kupata ‘order’ nyingi ya kupeleka bidhaa hiyo Kenya.
Lankii anasema baada ya kuona anapewa ‘order’ nyingi, alinunua eneo Tabata na kujenga ghala kwa ajili ya kukusanya, kuanika na kufunga mizigo yake ili aweze kusafirisha kwa urahisi.
“Namshukuru Mungu biashara yangu inaendelea vizuri, nimeongeza wafanyakazi kutoka watatu hadi 20.
“Nafikiri juhudi na malengo katika biashara yangu ndiyo imenifanya niwe mfanyabiashara wa Afrika Mashariki ninayeaminiwa na wateja wangu ninaponunua na kuuza pumba,” anasema.
Ili kuhakikisha shughuli zake anaziendesha kwa teknolojia ya kisasa, Lankii anasema amekwenda Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) kununua mashine ya kukausha na kufunga pumba.
“Mashine niliyoichukua Sido inanisaidia sana katika shughuli zangu kwa kuwa inakausha tani tano kwa siku… lakini nina mpango wa kuagiza mashine kubwa zaidi itakayoweza kukausha tani 20 kwa siku na kufanya shughuli za kupakia,” anasema.
Pamoja na mpango huo, Lankii anasema amejipanga kuanza kazi ya kusindika chakula cha kuku kwa ajili ya biashara katika soko la ndani na nje ya nchi.
“Nikiwa katika maandalizi ya kuanza kusindika chakula cha kuku kwa ajili ya kuwauzia wafugaji wa ndani na nje… nami najipanga kuanza kazi ya ufugaji wa kuku wa nyama na mayai kwa ajili ya biashara,” anasema.
Kwa kuwa kila kazi ina changamoto, Lankii anasema katika ujasiriamali anapambana na changamoto mbalimbali ikiwamo kupandishiwa tozo ya kibali cha kuvusha bidhaa zake kutoka nchini kuingia Kenya.
“Kwa kweli changamoto kubwa inayotukabili ni ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutupandishia tozo ya kibali kutoka sh 10,000 kwa gari lenye uwezo wa kupakia tani zaidi ya 20 hadi sh 10,000 kwa tani moja ambapo ukisafirisha gari la tani 30, utatakiwa kulipa sh 300,000,” anasema.
Lankii anasema changamoto nyingine ya bidhaa hiyo ni kuoza kwa pumba, hasa nyakati za masika na kusababishia hasara.
“Naiomba serikali yetu itupunguzie tozo ya kibali cha kusafirisha bidhaa zetu kwa kuwa tunapata faida ndogo… Watanzania na Waganda tunagombania soko hilo la Kenya,” anasema.
MTANZANIA

Maoni 3 :

  1. habari, nimesoma masiliamali ismail lankil nimevutiwa naye name pia ni mjasilia mali nipo msumbiji mr herman no +25882828268795 naomba no yake tuwasiliane kibiashara

    JibuFuta
  2. NIMEVUTIWA MNO NA MAELEZO YAKO JUU YA BIASHARA YA KUKAUSHA NA KUUZA PUMBA. NAOMBA MAWASILIANO YAKO KWA MAELEZO ZAID

    JibuFuta
  3. kwa mtu yeyote mwenye utaalamu juu ya utengenezaji wa chaki za mashuleni tuwasiliani 0718 316177

    JibuFuta