Shambulizi Gaza laua watu 15 katika soko
Takriban watu 15 wameuwa na wengine 160 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi kali la angani lililotekelezwa na Israeli kwenye soko moja huko Gaza .
Kwa mjibu wa viongozi wa Kipalestina mlipuko mkubwa ulilipua soko moja la Shejaiya la kuuza matunda na mboga ambalo kwa kawaida huwa na idadi kubwa ya watu, mashariki mwa Gaza.
Msemaji wa wizara ya afya Nchini Palestina amesema kuwa idadi kubwa ya wapalestina waliouwawa ama kujeruhiwa walikuwa wakiendesha shughuli za ununuzi wa bidhaa.
Msemaji wa kundi la Hamas, linalothibiti maeneo hayo Sami Abu Zuhri amekatalia mbali muafaka wa amani na kutaja kuwa hauna maana.
Wanahabari wanasema kuwa haijafahamika bayana iwapo wapalestina walikuwa wakijua kuwa watashambuliwa.
Shambulizi Gaza laua watu 15
Walioshuhudia wanasema kuwa, waliona moshi mkubwa ukifuka kutoka eneo hilo huku magari ya kutoa huduma ya kwanza yakionekana yakiingia na kutoka mahalipa tukio.
Aidha inasemekana kuwa mmoja wa waandishi habari ameuwawa katika shambulio hilo.
Wakati huo huo, majeshi wa nchi kavu ya Israel yamesema yatasitisha mapigano kwa muda wa masaa manne, lakini kauli hiyo haitotumika katika maeneo ambako wanajeshi wake wanaendeleza operesheni.
BBC
KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Jumatano, 30 Julai 2014
ISRAEL YAENDELEA KUWAUA WAPALESTINA

Jumamosi, 26 Julai 2014
MASKINI:MUNGU AMLAZE DR KAPOLI MAHALI PEMA
TANZIA!!!
Tumempoteza Mwalimu wetu Dr. Kapoli.
Hakika tutamkumbuka kwa changqmoto za kitaaluma alizokuwa akitupa tukiwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza SJMC-UDSM!
"Dr.KAPOLI AMEFARIKI DUNIA JANA KTK HOSPITAL YA TUMBI. TAARIFA HII NIMELETEWA NA MKE WAKE ASUBUHI SAA 2.00 ASUBUHI YA LEO 26.7.2014 MWL.ERNEST MRUTU"
"

HOSPITALI YA IMTU YAFUNGIWA BAADA YA SAKATA LA VIUNGO
Baadhi ya viungo vya miili vilivyokutwa
Oliver Oswald na Adam Malinda, Dar es Salaam
SERIKALI imeifungia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Tiba na Teknolojia (IMTU) kilichopo Mbezi eneo la Interchiki kwa muda usiofahamika.
Hospitali hiyo imefungiwa kutokana na kukosa sifa, ambapo imebainika kuwa maabara pamoja na wauguzi wake hawana vigezo vya kutoa huduma za kitabibu.
Hatua ya kuifungia hospitali hiyo imekuja siku chache tangu chuo hicho kilipokumbwa na tuhuma nzito za kuhusika na utupaji wa viungo vya binadamu katika eneo la Bonde la Mto Mpiji, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi jana, Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja, alisema Serikali imechukua uamuzi huo baada ya kugundua kasoro nyingi zinazoikabili hospitali hiyo.
Alisema katika ukaguzi uliofanywa na jopo la wataalamu kutoka wizarani kwa kushirikiana na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni, ulibaini kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kuendesha huduma za kitabibu.
“Kweli nimepokea taarifa za kufungiwa kwa Hospitali ya IMTU kutoka katika jopo letu lililokwenda kufanya uchunguzi hospitalini pale ambao wana wajibu wa kutembelea hospitali zote zilizopo ndani ya halmashauri yao kila mara.
“Katika uchunguzi wao wamethibitisha kukuta mapungufu hayo pamoja na mengine ambayo wizara itayaweka wazi katika mkutano wake na waandishi wa habari kesho (leo),” alisema Mwamwaja.
Aliyataja baadhi ya mapungufu yaliyogunduliwa na jopo hilo kuwa ni pamoja na hospitali hiyo kutokuwa na maabara inayojitosheleza kwa shughuli mbalimbali za kujifunzia pamoja na baadhi ya wauguzi wake kukosa sifa ya kutoa huduma za kitabibu.
Katika uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi ilibainika kuwa Chuo Kikuu cha IMTU kilihusika na tuhuma za kutupa mabaki ya viungo vya miili ya binadamu vilivyookotwa Julai 22, mwaka huu katika Bonde la Mto Mpiji.
Katika tukio hilo jumla ya mifuko 85 yenye viungo vya binadamu vilivyokaushwa na kuchunwa ngozi viliokotwa, ambapo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwatia nguvuni watumishi wanane kwa kuhusishwa na tukio hilo.
Viungo vilivyookotwa katika eneo hilo ni pamoja na mafuvu ya vichwa, sehemu ya kifua cha binadamu, miguu, mikono, moyo na mbavu.
Kwa upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi wa udaktari wa IMTU, Meekson Mambo, ameelezea kusikitishwa na uamuzi huo wa Serikali, akisema umewaathiri wanafunzi.
Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi jana muda mfupi kabla ya gazeti hili halijaenda mtamboni, Mambo alisema kufunga hospitali hiyo ni sawa na kufunga chuo kwa kuwa mafunzo ya vitendo hufanyika katika hospitali hiyo.
“Sisi tunaonewa katika sakata hili kwa kuwa waliofanya uzembe ni viongozi, hatuhusiki kwa namna yoyote na utupwaji wa mabaki ya miili hiyo iliyokutwa huko Mpiji. Kwa kweli uamuzi huu haukuzingatia athari tutakazozipata,” alisema.
Mambo alisisitiza kuwa Serikali inapaswa kuwa makini katika uamuzi inaoufanya, kwani wanafunzi wamebakiza muda mfupi kabla ya kuanza kwa mitihani ya kumaliza mafunzo.
Rais huyo alisema uamuzi huo wa Serikali haukuzingatia umuhimu wa wanachuo kupata haki ya masomo na mafunzo kwa njia ya vitendo, hivyo utawaathiri kisaikolojia.
“Tumebakiza muda mfupi, Agosti 4 mwezi ujao tunaanza mitihani, kama hospitali imefungwa hatima yetu ya mitihani itakuwaje, hii ni kujenga mazingira ya kufanya vibaya katika mitihani yetu,” alisema.
Hata hivyo, Mambo alishauri waliohusika na sakata hilo wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria ili kulinda heshima ya taaluma bila kuathiri wasio husika hasa wanafunzi waliopo chuoni hapo.
Mtanzania

Ijumaa, 25 Julai 2014
HATIMAE MTOTO ALIEIBWA CHANGANYIKENI APATIKANA.
HATIMAYE kinara wa wizi wa watoto jijini Dar es Salaam, Amir Juma, amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa mkoani Tanga.
Juma anadaiwa kumuiba mtoto, Merlin Repyson (4) katika eneo la Changanyikeni siku nane zilizopita.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo akiwa wilayani Korogwe

Jumatano, 23 Julai 2014
UNYAMA
CHUO Kikuu cha Kimataifa Matibabu na Teknolojia (IMTU) kilichopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam ndicho kinahusika na tukio la kinyama la kuichuna, kuikatakata, kuikausha na kisha kuitupa miili ya binadamu kwenye Bonde la Mbweni Mpiji, lililopo Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo awali gazeti hili lilizipata na kuthibitishwa na polisi pamoja na uongozi wa chuo hicho ni kwamba, chuo hicho ndicho kinahusika na sakata hilo na kwamba tayari baadhi ya viongozi wa chuo wameshakamatwa na Jeshi la Polisi.
Jana gazeti hili liliandika taarifa iliyoelezea tukio hilo kubainika baada ya akina mama wanaofanya kazi ya kuponda kokoto kwenye eneo hilo kufungua baadhi ya mifuko hiyo iliyokuwa imetupwa na watu wasiojulikana.
Mashuhuda wa tukio hilo walilieleza gazeti hili kwamba, viungo hivyo vya binadamu vilitupwa Julai 20, mwaka huu, lakini hakuna aliyegundua kutokana na kukaushwa na kupulizwa dawa iliyovizuia kutoa harufu.
UONGOZI WA CHUO WAKIRI
Ofisa Rasilimali watu wa Chuo hicho, Michael Lazaro, alikiri chuo chao kuhusika kwenye tukio hilo, lakini alishindwa kufafanua kwa kina ni kwanini walifanya hivyo, ambapo alisema kitengo cha maabara kinachohusika na uchunguzi na utafiti wa viungo vya binadamu ndicho kinahusika moja kwa moja na tukio hilo.
Lazaro alisema kwa mujibu wa taratibu za chuo, mabaki ya tafiti na chunguzi hizo huwa yanachomwa kwenye tanuru maalumu la kuchomea kemikali, lililopo Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo anashindwa kufahamu ni kwanini kitengo hicho kilikwenda kutupa taka hizo porini bila kutoa taarifa za kwanini hawakupeleka mabaki hayo Muhimbili.
Alipoulizwa ni wapi wanatoa miili hiyo, Lazaro alisema mtu pekee ambaye angeweza kutoa ufafanuzi wa kina wa wapi inatoka miili hiyo ni Mkuu wa kitengo hicho, anayefahamika kwa jina la Dimesh Kumaar, ambaye anashikiliwa na polisi.
Alipotakiwa kutupeleka kwa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Prabhakar Rao ili kuelezea sakata hilo, Lazaro alisema bosi wake huyo ni mgeni nchini, lakini pia naye ni mmoja wa viongozi wa chuo waliokamatwa na Jeshi la Polisi.
MADUDU YA CHUO YAIBULIWA
Baada ya tukio hilo, kumeibuka madudu mengi yanayokihusisha chuo hicho na sakata la kutupa viungo vya binadamu, ambapo mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho alisema uongozi wa chuo hicho umekuwa na matatizo na kwamba sakata kama hilo liliwahi kutokea miaka ya nyuma, ambapo kuna mwanafunzi wa chuo hicho alionekana akiwa na mkono wa binadamu mtaani kitendo ambacho hakiruhusiwi.
Mtoa habari wetu alisema kuwa muhula wa kwanza wa masomo ulimaliza kutumia miili hiyo mwezi Machi mwaka huu na uongozi ulitakiwa kuiteketeza, lakini walishindwa kutokana na kifaa cha kuteketeza mabaki hayo kuharibika, ambapo waliomba msaada Muhimbili, huko nako waliambiwa kifaa kimeharibika.
Katika kuhakikisha wanaviteketeza inadaiwa waliomba msaada kwenye maeneo mbalimbali, ambapo walitakiwa kutoa fedha ili kazi hiyo ikamilike, lakini walishindwa kutoa fedha badala yake wakaamua kwenda kuitupa bondeni.
Alisema kuwa hatua hiyo ilifikiwa ili kuwahadaa wajumbe waliokuwa kwenye msafara wa Umoja wa Vyuo vya Madaktari Afrika, ambao kama wangekutana na mabaki hayo ni wazi wangepoteza sifa.
MUHIMBILI WAZUNGUMZA
Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminieli Eligaesha, alikiri kuharibika kwa mtambo wa kuteketeza mabaki hayo hata hivyo alikanusha uvumi wa kwamba viungo hivyo vimetoka hospitalini hapo.
Eligaesha alisema kifaa hicho kimeharibika tangu mwezi Februari mwaka huu na kwamba waliagiza kifaa kingine kutoka nje ya nchi ambacho baada ya kuunganishwa kifaa kingine kiliharibika.
“Kawaida huwa tunaagiza vifaa vya mitambo yetu kutoka nje ya nchi, lakini tulipounganisha kuna kifaa kingine kiliharibika na ndiyo maana hadi sasa ndugu waandishi mmeshuhudia mafundi wakiendelea kuutengeneza mtambo huo na kwa mujibu wao utakuwa tayari hivi karibuni,” alifafanua Eligaesha.
JESHI LA POLISI LAUNDA JOPO LA UCHUNGUZI
Kwa upande mwingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limeunda jopo la upelelezi la watu saba linaloongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Japhari Mohamed.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alisema jopo hilo limeshaanza uchunguzi mara baada ya kupata taarifa hizo kwa kushirikiana na Daktari wa Jeshi la Polisi ambaye anahusika na uchunguzi wa miili ya binadamu pamoja na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Kova alisema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa kwa mara ya mwisho viungo hivyo vilikuwa katika maabara ya Chuo Kikuu cha Madaktari cha International Medical and Technological University (IMTU) kilichopo jijini Dar es Salaam ambacho pia hufanya mafunzo ya udaktari kwa vitendo.
Alisema jeshi hilo tayari linawashikilia watu wanane kwa mahojiano kutokana na utupwaji wa viungo hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alisema viungo hivyo vilipatikana jana katika eneo hilo vikiwa katika mifuko mieusi ya plastiki ipatayo 85.
Alisema kati ya watu wanane waliokamatwa wengine ni madaktari pamoja na wale waliohusika katika utekelezaji wa tukio hilo na wamewahoji na kukiri kuhusika.
“Miongoni mwa maswali tutakayoendelea kuwahoji ni pamoja na sababu ya wingi wa viungo hivyo na kwanini walienda kuvitupa katika eneo lile la wazi ambalo watu wengi hupita.
“Ili kufanikisha upelelezi wetu, tutamshirikisha Mkemia Mkuu wa Serikali ili aweze kufanya uchunguzi wa kina ikiwamo kubaini viungo hivyo ni vya muda gani kwa kutumia vinasaba (DNA), pia itabainika kuwa ni vya watu wangapi.
“Baada ya uchunguzi kukamilika jalada hilo litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili hatua za kisheria zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika pamoja na kujua kuwa ni sheria gani zimevunjwa katika kulinda viungo vya binadamu,” alisema Kova.
MAITI ZINAVYOPATIKANA
Wataalamu wa afya wameeleza namna miili hiyo inavyopatikana na kutunzwa kwa ajili ya mafunzo.
Wamesema kuwa miili hiyo hupatikana kutokana na maiti ambazo zimekaa kwa kati ya miezi sita mpaka mwaka bila kutambuliwa na ndugu zao.
Walisema miili hiyo hutoka katika nchi mbalimbali na kwamba nchi moja ikiwa na shehena ya maiti hutafuta nchi nyingine iliyo mbali ili kubadilishana miili hiyo.
“Kwa mfano Tanzania inaweza kubadilishana miili hii na nchi nyingine iliyo Afrika Magharibi, vinapofika vyuoni huwekwa kwenye maabara maalumu, jambo hili hufanyika kwa umakini sana, haijawahi kutokea mtu aliyeenda kusomea fani ya tiba akakutana na mwili wa ndugu yake ama rafiki yake,” alisema Dk. Samwel Shita.
Dk. Shita ambaye ni mtaalamu wa tiba, anasema miili hiyo hujulikana kitaalamu kama cadaver na hutumiwa na wanafunzi wa vyuo vya tiba, lengo likiwa ni kuifanyia upasuaji ili kujifunza maumbile ya mwili mzima wa binadamu.
Anasema kuwa miili hiyo inaweza kuwa ni ile iliyokosa ndugu wa kuizika na pia baadhi ya watu hujitolea na kuandika kimaandishi kuwa pindi wakifariki miili yao itumike kwa ajili ya mafunzo.
Anasema baada ya kukamilika kwa zoezi hilo hupendekeza namna ya kuhifadhiwa kwake, maiti hizo huhifadhiwa kwa kipindi cha miezi sita mpaka mwaka mmoja kisha kukabidhiwa kwa wataalamu wa afya ambao huzitunza na kuziwekea dawa maalumu ili zisiharibike wala kuguswa na bakteria wa aina yoyote.
Dawa hiyo inajulikana kama 2-phenoxethanol maarufu kama fomulani. Anasema kuwa dawa hii huingizwa katika mshipa mkubwa wa paja na kisha huenea sehemu yote ya mwili kupitia mfumo wa mishipa ya damu.
Anasema kuwa dawa hiyo huweza kuutunza mwili huo kwa muda mrefu na kuwa hakuna vijidudu vinavyoweza kuugusa na hata ukiwekwa sehemu ya wazi hakuna ndege wala mnyama atakayeweza kuugusa.
“Si kunguru, bakteria au fangasi au kiumbe chochote kinachoweza kuugusa au kuishi kwenye mwili uliowekwa dawa hii,” alisema Dk. Shita.
Alisema kuwa dawa hiyo inatambulika kama moja ya kemikali zinazoweza kusababisha saratani kama mtu atakumbana nayo kwa muda mrefu.
Dawa hii huweza kuwa na harufu kali na inayokera, ina ukakasi na pia huwa rahisi kuwa kama mvuke ambao mtu akiuvuta hupata shida kupumua.
Baada ya mwili huu kutengenezwa, huifadhiwa katika vyombo maalumu vilivyojaa dawa ya maji ya fomulani mpaka pale itakapohitajika.
Dk. Shita anaeleza kuwa mwili wa binadamu umefunikwa kwa ngozi ambayo huwa ni ngumu, hivyo hulazimu watu wanaojifunzia miili hiyo kutenganisha ngozi kwa kuichuna ili kuweza kuona sehemu za mwanzo ambazo huwa na tishu laini kama kitambaa na sehemu hizo huitwa farcia.
Pia huweza kuonyesha mishipa ya damu kwa juu, mishipa ya fahamu ilivyogawanyika katika tishu, misuli ya mwili pamoja na viungo vingine.
Anasema kuwa ni vigumu kuzifikia sehemu hizo bila kuchuna ngozi.
Anasema kuwa dawa ya fomulani husababisha athari mbalimbali katika mfumo wa hewa, mfumo wa fahamu na ngozi.
Alisema kuwa dawa hiyo ndiyo inayonyima kiumbe chochote kuweza kuishi.
Wakati Dk. Shita akieleza namna miili hiyo inavyopatikana na kutunzwa, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Tiba cha Bugando, Dk. Rodrick Kabangila, anasema hata kama miili hiyo ilitumika kwa ajili ya kufundishia wanafunzi wa tiba, kuitupa porini kunaonyesha namna mamlaka zinazosimamia fani hiyo zilivyoshindwa kufanya kazi.
“Mimi nilivyoona hiyo shehena nilikuwa na mambo mawili ya kujiuliza, kwanza niliona yawezekana yametoka hospitali ama kwenye vyuo vya tiba ambapo wanafunzi hutumia kujifunzia.
Lakini ukiangalia hata kama imetoka kwenye vyuo huwa kuna namna ya kuihifadhi kazi yake ikiisha. Nilivyoona zile ngozi zilivyokuwa nyingi nikasema ni vigumu zikawa zimetoka hospitali kwa sababu kule huwa wanachukua ngozi kidogo tu kwa sababu ya kuziweka kwenye sehemu nyingine ya mwili,” alisema Dk. Kabangila.
Alisema kuwa tangu miaka ya 1970 madaktari wamekuwa wakifundishwa na hakuna tukio kama hili, hivyo yawezekana kilichofanyika ni hujuma ama waliopewa kuteketeza mzigo huo walitaka kwenda kuuza.
“Yawezekana watu walikula hela ama ni mtu alikuwa amepatana na mtu mwingine ampelekee huo mzigo wakashindwa kuelewana bei ndiyo wakaenda kuutupa huko,” alisema.
Alisema kuwa katika kufundisha wanafunzi wa udaktari, ni suala la kawaida kuchuna ngozi ya sehemu moja ili kujua mishipa ya damu imepita wapi, ikoje, misuli imepita wapi na ikoje.
Habari hii imeandaliwa na Asifiwe George, Veronica Romwald, Deonidas Mukebezi na Jonas Mushi
MTANZANIA

Jumanne, 22 Julai 2014
WATU NANE MASHAKANI SAKATA LA VIUNGO VYA BINADAMU
Watu hao ambao ni pamoja na madaktari wa hospitali ambayo pia ni chuo cha udaktari IMTU kilichopo jijini Dar es salaam wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya uchunguzi wa awali ambao umebaini kuwa mifuko hiyo ilitoka katika hospitali hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari,kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema kuwa viungo hivyo havikuwa na uvundo wala harufu yoyote na vilionekana kuwa vimekaushwa na kukakamaa.Kova alisema pia kuwa katika eneo hilo vilionekana vifaa vinavyotumika hospitari kama vile mipira ya kuvaa mikononi(gloves) nguo maalum(apron) na mifuko miwili iliyotunika pamoja na karatasi mbili zenye maswali na majibu.
"Viungo hivyo vilichukuliwa na kupelekwa muhimbili kwa uchunguzi zaidi na jopo la wapelelezi wakiongozwa na mkuu wa upelelezi kanda maalum ACP Japhar Mohamed walianza upelelezi mala moja kwakushirikiana na daktari wa jeshi la polisi anayehusika na uchunguzi wa miili ya binadamu(forensic Doctor) ambaye alishilikiana na madaktari wengine kutoka hospitali ya taifa Muhimbili"Alisema Kova
Kamanda Kova aliongeza kuwa baada ya uchunguzi ilibainika kuwa viungo hivyo kwa mala ya mwisho vilikuwa katika maabara ya chuo kikuu cha madaktari IMTU ambacho pia hufanya mafunzo ya udaktari kwa vitendo.
Kamanda Kova alisema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea na jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote ambae atagundulika kuhusika na tukio hilo na kuwataka wananchi watulie wakati polisi ikiendelea na uchunguzi
Alhamisi, 17 Julai 2014
MTOTO WA MIAKA SITA ABAKWA NA WATU WAWILI
Polisi Kusini mwa India wamesajili kesi ya ubakaji ambapo inaarifiwa mtoto wa shule mwenye umri wa miaka 6 alibakwa na wafanyakazi wawili wa shule moja maarufu mjini Bangaloer.Kisa hicho kinaarifiwa kutokea wiki mbili zilizopita.
Mtoto huyo alibakwa na mlinzi pamoja na mwalimu, lakini kwa sababu ya kuwepo walinzi wengi katika shule hiyo, polisi bado wanachukua muda kuchunguza mlinzi aliyehusika.
Polisi wanasema kuwa mtoto huyo alibakwa tarehe mbili Julai , lakini wazazi wake waligundua hilo siku chache zilizopita baada ya mtoto huyo kulalamika kuumwa na tumbo na kupelekwa hospitalini.
Wakati huo mamia ya wazazi wameandamana nje ya shule wakivunja milango na kupiga mayowe kulaani tukio hilo.
Polisi tayari wamesajili kesi hiyo , lakini bado hawajamkamata mtu yeyote.
Mwandishi wa BBC Andrew North mjini Delhi anasema kuwa tukio hilo ni la hivi karibuni kugonga vichwa vya habari nchini India.
Waziri mkuu Narendra Modi, ameahidi kupambana vilivyo na visa vya ubakaji, na udhalilishaji wa kijinsia , lakini unyanyasaji wa wanawake bado ni tatizo kubwa sana nchini humo.
Huku taarifa ya kubakwa kwa mtoto huyo zikijitokeza tu, mamia ya wazazi walikusanyika nje ya shule hiyo na kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya wasimamizi wa shule.
Mnamo siku ya Alhamisi mwenyekiti wa shule Rustom Kerawala alizungumza na wazazi ambapo aliomba msamaha na kuahidi kushirikiana na polisi katika uchunguzi.

KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA
MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2014 YATOKA
Matokeo ya mtihani wa kidato cha 6 yaliyofanyika tarehe Mei 5 – 21, yametoka.Jumla ya watahiniwa 38,905 sawa na asilimia 95.98 ya watahiniwa waliofanya mtihani kidato cha 6 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 12,080 na wavulana waliofaulu ni 26,825.
Watahiniwa waliopata division IV ni 4,420 sawa na asilimia 12.54
Watahiniwa waliopata zero (0) ni 612 sawa na asilimia 1.74.
SHULE 10 ZILIZOONGOZA
1. Igowole
2. Feza Boys
3. Kisimiri
4. Iwawa
5. Kibaha
6. Marian Girls
7. Nangwa
8. Uwata
9. Kibondo
10. Kawawa
SHULE 10 ZA MWISHO
1. Ben Bella
2. Fidel Castro
3. Tambaza
4. MuhezaHigh School
5. Mazizini
6. Mtwara Technical
7. Iyunga technical
8. Al- falaah Muslim
9. Kaliua
10. Osward Mang'ombe
Kuona matokeo pitia hapa: http://www.necta.go.tz /matokeo2014/ACSEE.htm
MATOKEO KIDATO CHA 6: 95.98% wafaulu kidato cha 6 kutoka 87.9% mwaka jana. Tambaza ndani ya shule 10 za mwisho, K/Katibu Mtendaji Necta C. Msonde atangaza leo.

Jumatatu, 14 Julai 2014
KOCHA WA BRAZIL AJIUZULU
Scolari amelaumiwa kwa kichapo ilichopata Brazil
Ripoti nchini Brazil zinasema kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil,Luiz Felipe Scolari, ameacha kazi kama meneja wa timu hiyo.
Scolari alilaumiwa pakubwa sana kwa timu ya Brazil kupata kichapo kibaya ilipocheza na Ujerumani ambao wameibuka mabingwa wa kombe la dunia mwaka huu.
Kichapo hicho kilikuja wakati wa mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani.
Taarifa rasmi huenda ikatolewa baadaye leo na shirikisho la soka la Brazil.

Alhamisi, 10 Julai 2014
KIKWETE AMWAMBIA MAKAMBA AACHE PAPARA
Rais Jakaya Kikwete amezungumzia nia ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba kutaka kuwania urais mwakani, akisema mwanasiasa huyo kijana “anataka mambo makubwa, lakini hajamshirikisha”.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Kikwete kutoa maoni yake kuhusu wanachama wa CCM wanaotaka kuwania urais, baada ya chama hicho kuwaonya makada sita kwa tuhuma za kuanza mapema kampeni za kutaka nafasi hiyo kubwa.
Akiwa jijini London, Makamba alitangaza nia yake ya kuwania urais mwaka 2015, akisema huu ni wakati wa fikra mpya ambazo zinahitaji vijana na kwamba wazee wakae kando.
Jana, Rais Kikwete, ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Soni Bumbuli mkoani Tanga anakoendelea na ziara ya siku tano, alimtaka Makamba “asilazimishe” kwa kuwa wakati ukifika atapata kile anachokitaka.
“Nasikia kuwa bwana mdogo January anataka mambo makubwa. Mie hajaniambia, na mie nasikia. Hata alipogombea ubunge hakuniambia nilisikia baadaye... asilazimishe, wakati ukifika atapata, na akikosa asilete nongwa,”alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alitoa mfano wake mwenyewe aliposhindwa katika uteuzi wa mgombea urais wa CCM mwaka 1995, wakati akiwa na miaka 45 (miaka minne zaidi ya umri wa Makamba ifikapo 2015), akisema kuwa hakukata tamaa na aliendelea kusikiliza ushauri wa wazee hadi alipofanikiwa kukalia nafasi hiyo ya juu mwaka 2005.
Mwenyekiti huyo wa CCM, ambaye pia ushawishi wake unaweza kuamua mteule wa chama, alimtaka mbunge huyo wa Bumbuli asikilize ushauri wa wazee.
Pamoja na ushauri huo kwa mwandishi wake wa zamani wa hotuba, Rais Kikwete alimpongeza kwa kazi nzuri ya ubunge jimboni humo na akaeleza kuwa anamsaidia katika wizara yake.
Alinukuu maneno ya aliyekuwa katibu mkuu wa Afro Shiraz na swahiba wake, Thabit Kombo aliyemwambia Kikwete kuwa “wakati ukifika utapata”, hasa kutokana na kiu yake ya muda mrefu ya kuwatumikia Watanzania.
“Nilipokosa mwaka 1995 sikukata tamaa, ndipo 2005 nikaingia, na huo ndio ulikuwa wakati wangu wa kushika wadhifa huu. Wakati ukifika watu watake wasitake utakuwa wewe tu,”alisema Kikwete.
Kauli hiyo ya Rais Kikwete imekuja takriban wiki moja baada ya Makamba kueleza nia yake ya kuwania urais akisema kwa asilimia 90 ameshaamua kuingia katika kinyang’anyiro hicho.
Mbunge huyo wa Bumbuli, ambaye ni mtoto wa Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba, alitangaza uamuzi huo akiwa Uingereza alikokuwa akihudhuria mkutano wa sekta ya mawasiliano baada ya kuhojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na baadaye kufafanua nia hiyo katika mahojiano na gazeti hili.
Rais Kikwete akimshauri asikilize ushauri wa wazee, wakati akitangaza nia hiyo Makamba alisema:“Ni wakati wa fikra mpya kushika dola na mimi ninaona kwamba wazee wakae kando. Mfano awamu moja inapoondoka na wazee walioko katika mfumo wakae kando ili kupisha fikra mpya kuongoza dola.”alisema Makamba ambaye kwa sasa ana miaka 40.
Makamba ameendelea kusisitiza nia yake hiyo na kutetea nafasi ya vijana katika nafasi hiyo kwenye ukurasa wake wa facebook akisema: “Tanzania mpya inahitaji viongozi wapya, mazoea mapya, fikra mpya na maarifa mapya. Inahitaji kuthubutu mambo makubwa siyo kulinda uzoefu wa nyuma.”
Makamba ni mmoja wa makada sita wa CCM walioonywa na chama hicho mapema mwaka huu kwa kutuhumiwa kuanza mapema kampeni za urais kinyume na utaratibu, lakini chama hicho hakijaona kasoro katika uamuzi wake wa kutangaza nia.
CCM yambariki
Katika hatua nyingine, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimebariki mbio za Makamba baada ya jana kueleza kuwa hajafanya kosa lolote kwa kutangaza nia yake.
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema alichofanya Makamba ni tofauti na adhabu ambayo chama hicho kilimpa yeye na wenzake watano miezi mitano iliyopita.
Nape aliwataka wanaohoji suala hilo kurejea adhabu iliyotolewa na CCM, Februari 18, mwaka huu kwa makada wake sita baada ya kukutwa na makosa ya kuanza mapema kampeni za urais mwaka 2015, akiwamo Makamba.
Wengine waliokutwa na rungu hilo ni mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe na William Ngeleja.
“Hili jambo linakuzwa tu wakati katika barua tulizowapa tulieleza wazi. Waambie wawaonyeshe barua ambazo chama kimewapa ili mjue nini ambacho hawatakiwi kukifanya,”alisema Nape.
“Yeye amesema akipewa ridhaa ya kugombea urais, jambo hili halipo kati ya makosa ambayo yalisababisha yeye na wenzake kupewa adhabu.”
Februari 18, mwaka huu Kamati Kuu ya CCM ilitoa adhabu kwa makada hao baada ya kuthibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea urais kabla ya wakati kinyume na kanuni za uongozi na uaadili za chama hicho.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula aliwahi kukemea tabia ya baadhi ya wana-CCM kutangaza mapema nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao, akisema ni wasaliti wakubwa ndani ya chama.
CCM pia ilitoa mwongozo na kanuni za uchaguzi ambazo Ibara 6 (2) (1-5) ya Maadili ya Viongozi wa CCM inawazuia wanachama kutoa michango, misaada, zawadi za aina yoyote, kukusanya michango na kufanya kampeni bila ya kupata kibali kutoka kamati ya siasa ya halmashauri ya eneo husika.
Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni za uongozi na maadili za CCM, toleo la Februari 2010, Ibara 6 (7)(i), ni kinyume kwa wanachama wake kutafuta kuteuliwa kuwania urais kabla ya wakati.
Credit: Mwananchi

Jumanne, 8 Julai 2014
SOMA
DONDOO 8 MUHIMU KWA WAZAZI NA WAZAZI WATARAJIWA
1. Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha
unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu
2. Mkanye mtoto wako wa kike kuhusu kukubali kupakatwa hovyo,
bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.
3. Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao “Mchumba”, “Mke wangu” au “Mme wangu”.
4. Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi.
Jifunze kumwomba akupishe.
5. Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwenda kwa mtu fulani
usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.
6. Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.
7. Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.
8. Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya fuatilia ujue sababu ni ipi.

Jumatatu, 7 Julai 2014
UJASIRIAMALI UNA BADIRISHA MAISHA
UJASIRIAMALI una maana pana, miongoni mwa hizo ni kuwa na hamasa kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika uchumi.
Pia katika hali nyingine mjasiriamali anaweza kuwa mtu yeyote anayejishughulisha katika sekta fulani, mfano kilimo, ufugaji au biashara.
bonyeza hapa kusoma zaidi..

UTAFITI NI MUHIMU KATIKA BIASHARA
WATU wengi hufikiri kwamba mtaji ni kigezo pekee cha kuanzisha biashara na kutoona umuhimu wa kufanya utafiti.
Kutokana na hali hiyo, hujikuta biashara zao zikishindwa kuhimili ushindani kwa kuanguka au kukosa wateja.
Unapozungumzia utafiti, watu huchukulia ni masuala makubwa kama ya kisayansi jambo ambalo si kweli.
Utafiti wa kibiashara ni utafiti unaohusu mambo madogo madogo yanayoweza kuathiri au kutoathiri biashara yako.
Ni vizuri ukayafahamu mambo hayo kabla na kujipanga namna ya kukabiliana nayo.
Utafiti ni suala la kulipa kipaumbele kabla ya kuanza biashara ili kumsaidia mfanyabiashara kuzifahamu changamoto za biashara husika anayoenda kuifanya.
Yapo maeneo muhimu ambayo mfanyabiashara anatakiwa kuyafanyia utafiti kabla ya kuanza biashara ambayo ni wateja, utafiti wa bei, washindani, mabadiliko ya tabia ya nchi, magonjwa na hali ya siasa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Alpha Associate Ltd, inayojishughulisha na masuala ya ushauri kwa wafanyabiashara jijini Arusha, Alphonce Massaga, anasema ni vema mfanyabiashara akafanya utafiti wa wateja anaowategemea kununua bidhaa zake.
Mshauri huyo anagusia suala la utafiti iwapo bidhaa hiyo inakubalika katika jamii husika.
Pia kutazama mila na desturi za eneo husika iwapo zinaruhusu kuwepo kwa biashara husika.
Utafiti wa bei unaofanyika kabla ya kupanga bei ya bidhaa au huduma husika ili kuangalia kama bei hiyo itakubalika, pia unakwenda sambamba na utafiti wa hali ya uchumi wa watu wa eneo husika kwani ukishajua hali zao za kiuchumi ni rahisi kupanga bei inayoshabihiana na kipato cha watu wanaoishi karibu na biashara yako.
Kwa mtazamo wangu ni muhimu kujifunza mbinu wanazotumia wapinzani wako katika biashara. Hapa unapaswa kuangalia bei zao na ubora wa bidhaa ili kujua namna utakavyoshindana nao bila kuanguka kibiashara.
Suala la mbinu za kibiashara na siri zilizoko ndani ya biashara husika unayotaka kuanzisha unaweza ukajifunza kwa watu wanaofanya biashara kama yako walioko maeneo ya mbali.
Ukifanya hayo kwa wale walioko karibu wanaweza wasikupe ushirikiano kwa kuhofia kupitwa.
Pia utafiti wa maeneo ni muhimu kwani unamsaidia mfanyabiashara kugundua fursa zilizopo katika eneo husika ikiwemo mahitaji ya jamii kama chakula, mavazi, malazi, huduma za usafiri na afya ambazo humsaidia mjasiriamali kujua ni biashara gani aanzishe itakayompatia faida.
Pia inamsaidia mfanyabiashara kujua mila na desturi za jamii husika.
Mfano unataka kuanzisha biashara ya suti maeneo ya jamii ya Wamasai ambao wengi wao huvaa migorore (mashuka ya kimasai na vikoi), ni wazi kuwa hutopata wateja na biashara yako haitakuwa endelevu. Hivyo ni vema utafiti wa maeneo ukazingatiwa.
Vilevile katika biashara utafiti juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi ni muhimu sana, hasa kwa wale wanaofanya biashara ya mazao ya kilimo, linapokuja suala la ukame linaathiri sana biashara hiyo.
Utafiti huo utamsaidia mfanyabiashara kujua taarifa muhimu kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa au kutokana na utafiti alioufanya mwenyewe.
Massaga anasema unakuta mkulima alitarajia kulima hekari 50 ili apate faida, linapokuja suala la mabadiliko ya hali ya hewa linamuathiri kwa kiasi kikubwa pamoja na kupungua kwa kiwango cha uzalishaji, kwa hili wakulima wanaweza kulijua mapema wakifanya utafiti.
Ili kuwa na biashara endelevu inayohimili ushindani na yenye mafanikio, utafiti ni jambo la msingi sana la kuzingatia kabla ya kuanza biashara na baada ya kuanza biashara.

Jumapili, 6 Julai 2014
WASICHANA WATOROKA KAMBI YA BOKO HARAMU
Maafisa wa usalama wa Nigeria wamesema kuwa zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo wamekewpa kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram waliokuwa wamewateka nyara.
Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa kaskazni mashariki mwa jimbo la Borno.serikali ya Nigeria imeitisha kufanywe uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka wasichana hao.
wapiganaji wa Boko Haram
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi. Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa Ijumaa hiyo (4 Julai) walifanikiwa kuwaua wapiganaji zaidi ya 50 karibu na mji wa Damboa.
Bado wasichana wengine hawajapatikana
Hata hivyo bado wanamgambo hao wa Boko Haram wanawazuilia zaidi ya wasichana wengine 200 waliowateka nyara mwezi Aprili. Hatua ambayo imekemewa vikali na jamii ya kimataifa huku baadhi ya mataifa kama vile Marekani, Uingereza na hata Ufaransa wakijitolea kuisaidia serikali ya Nigeria kuwasaka wasichana hao.

Jumamosi, 5 Julai 2014
AMTUPA MTOTO KWENYE KICHAKA KINACHOWAKA MOTO NA KUMSABABISHIA KIFO
Kigoma.Mkazi wa Kijiji cha Muhunga kilichopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma (Gloria Rubeben(20) anashikiliwa na polisi mkoani humo kwa kumtupa mtoto wake wa siku nne katika kichaka na hatimaye kufa baada ya kuungua na moto uliowaka katika kichaka hicho.
Akithibisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Frasser Kashai alisema Julai 2, 2014 majira ya saa 3.00 usiku katika kijiji cha Muhunga wilayani Kasulu Rubeben alifanya ukatili huo kwa mtoto wake , ambapo majirani waligundua kitendo hicho na kutoa tarifa sehemu husika.
Kamanda Kashai alisema , uchunguzi bado unaendelea ili kujua kiini cha mama huyo kufanya tukio hilo.
Katika tukio lingine Mwanamke mmoja, mkazi wa kijiji cha Minyima wilayani Kibondo atafikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kigoma kujibu tuhuma za kumuua mumewe.
Alisema Julai 2, 2014 saa 2.00 usiku mwanamke huyo alimpiga mumewe na figa la jikoni baada ya mumewe kuhoji ujio wa wageni watatu waliokuwa wamefika nyumbani kwake.Hata hivyo, KamandaKashai aliwaomba wanancchi wazidi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
MWANANCHI

Ijumaa, 4 Julai 2014
SAFARI YA NEYMAR KOMBE LA DUNIA YAISHIA ROBO FAINAL:NDOTO YA KIATU CHA DHAHABU YAFUTIKA
Nyota wa timu ya soka ya Brazil Neymar hatoshiriki tena katika michuano ya kombe la dunia baada kupata jeraha.
Mfupa wake unaoshikana na uti wa mgongo ilivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia.
Neymar aligongwa upande wake wa nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika.
Alibebwa na kutolewa nje akiwa katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.
Brazil pia itaendelea kushiriki katika mashindano hayo bila nahodha wake Thiago Silva katika mchuano wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya Njano.
Kabla ya habari hizo za Neymar kutolewa raia wa Brazil walifurika katika barabara za taifa hilo kusherehekea ushindi wa timu yao.
Katika robo fainali ya kwanza Ujerumani iliishinda ufaransa kwa bao moja kwa bila .

UFARANSA OUT KOMBE LA DUNIA
Mfungaji bao la Ujerumani
Ujerumani Imesajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa katika mechi ya robo fainali.
Kufuatia ushindi huo dhidi ya Ufaransa ndiyo timu ya kwanza kuwahi kufuzu kwa nusu fainali katika mashindano manne ya kombe la dunia mfululizo .
Ujerumani ndiyo timu ya kwanza kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Kufuatia ushindi huo Ujerumani watakutana na mshindi baina ya Brazil na Colombia katika hatua ya nusu fainali .
90'30 Ujerumani 1-0 Ufaransa
85:35 Ujerumani 1-0 Ufaransa
58:50 Kadi ya kwanza ya manjano inamwendea Sami Khedira refarii Nestor Pitana amechoshwa na mchezo wake wa ngware .
57:34Depsome Elisha Kahama tz! Ujeruman bingwa
Bao la Mat Hummels
Samwel Paul: Ufaransa lazima watoke hata kupambana kwao kote Ujerumani
51:30Husein Mono Wa Mwanga Kilimanjaro TZ ;Ufaransa bado wanna uwezo hata was kushinda!
45:20 Kipindi cha pili kimeanza
45'' Kipindi cha kwanza kimekamilika .
44 Ujerumani 1-0 Ufaransa
41 Benzema anakosa fursa nyengine ya kuisawazishia Ufaransa.
40'' Mechi hii inaendelea katika uwanja wa kihistoria wa Maracana
Kufikia sasa Bao la dakika ya 12 la Mats Hummels ndilo linaipatia ujermani kipao mbele
Mshindi wa mechi hii atakutana na mshindi kati ya Brazil na Colombia katika nusu fainali.
Ujerumani inakabiliana na Ufaransa kutafuta tikiti ya nusu fainali ya kombe la dunia .

Alhamisi, 3 Julai 2014
KUHUSU VIJANA WATATU WANAODAIWA KUFA KUTOKANA NA KUFANYIWA UKATILI JKT.
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limekanusha taarifa zilizosambazwa kuwa vijana wa mujibu wa sheria, wanaoendelea na mafunzo katika kambi za JKT, kuwa wanakufa kwa ukatili.
Hayo yalisemwa jana na Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Erick Komba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema taarifa hizo potofu zimesambazwa kwa njia ya Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS) katika simu za mkononi na mitandao ya kijamii na zilidai kuwa Kambi ya JKT Oljoro Arusha kuna vijana watatu wamefariki.
Komba alisisitiza kuwa taarifa hizo si za kweli na ni upotoshaji kwa vijana wa Tanzania, kwani ukweli ni kwamba kijana mmoja pekee aliyejulikana kama Honorata Oiso, alifariki katika kikosi cha JKT Oljoro Arusha, kwa ugonjwa wa upungufu wa damu (anaemia), uliosababishwa na malaria na sio watatu kama ilivyoelezwa.
"Wazazi wa kijana aliyefariki walithibitisha kuwa kijana wao alikuwa na matatizo ya upungufu wa damu na sio ukatili, kama ilivyoelezwa na ujumbe uliokuwa ukitumwa kupitia mitandao ya kijamii,’’alisema Komba.
Alisema watu hao wameamua kutumia kifo cha kijana huyo, kusambaza uongo ambao haukubaliki katika jamii.
“Jeshi linasisitiza kuwa hakuna ukatili unaofanywa kwa vijana wanaoendelea na mafunzo katika kambi za JKT,”alisema.
Kwa mujibu wa Komba, hivi sasa JKT lina vijana 38,634 wanaoendelea na mafunzo. Kati yao ni wasichana waliopelekwa kwa mujibu wa sheria ni 5,446 na wavulana 12,822. Kwa upande wa wanaojitolea, wavulana ni 15,509 na wasichana 4,859.
Ofisa Habari wa JKT, Meja Emmanuel Muruga alisema hakuna mwanafunzi anayefanyiwa vitendo vya ukatili na wanafunzi wote waliojiunga kwa mujibu wa sheria, wanapimwa afya kabla ya kuanza mafunzo.
Aliongeza kuwa hata kama mtu atakuwa na ulemavu na ameenda kwa mujibu wa sheria, atafanya mazoezi kama kawaida na kama ana tatizo la afya, kama kifua na mengine, atatembea na wenzake wakikimbia, ila lazima ajumuike na wenzake.
Pia, alisema kwa wale wa kujitolea, kabla ya kujiunga ni lazima wafuate masharti ya JKT. Masharti hayo ni anapaswa kuwa na miaka 18-23, awe mtanzania na asiwe amewahi kuhusika na tukio lolote la uhalifu na akubali mwenyewe kujiunga na jeshi.
Alisisitiza kuwa JKT inalaani kitendo hicho na itafuatilia ili kubaini chanzo chake, na atakayebainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Alisema Jeshi hilo linawakumbusha vijana kuwa makini na matumizi mabaya ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii, hasa taarifa zinazohusiana na jeshi.

MAKAMBA KUGOMBEA URAIS 2015
Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ametangaza nia yake ya kuwania urais akisema huu ni wakati wa kupisha fikra mpya kuongoza dola, licha ya chama hicho kuzuia kutangaza nia na kupiga kampeni kabla ya muda.
Makamba, mmoja wa makada wa CCM walioonywa na chama hicho baada ya kutuhumiwa kuanza kampeni mapema, alijipigia debe kuwa iwapo atapitishwa na chama hicho, ataelekeza nguvu kwenye vipaumbele vyake vinne ambavyo ni ajira, huduma za jamii, uchumi imara na utawala bora.
Mbunge huyo wa Bumbuli alisema hayo akiwa Uingereza anakohudhuria mkutano wa sekta ya mawasiliano baada ya kuhojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza na baadaye kufafanua nia hiyo katika mahojiano na Mwananchi jana.
“Ni wakati wa fikra mpya kushika dola na mimi ninaona kwamba wazee wakae kando. Mfano awamu moja inapoondoka na wazee walioko katika mfumo wakae kando ili kupisha fikra mpya kuongoza dola,” alisema Makamba ambaye ana umri wa miaka 40.
Mwandishi huyo wa zamani wa hotuba za Rais Jakaya Kikwete, alisema hadi sasa ameshafanya uamuzi kwa asilimia 90 kujitokeza kuwania nafasi hiyo ya juu kuliko zote nchini, bado asilimia 10 katika baadhi ya mambo ambayo anaendelea kuyatafakari, kuzungumza na makundi mbalimbali ya wazee, viongozi wa dini na viongozi waliopita “ili nipate ushauri wao kuhusu namna ya kufanya jambo hili”.
Alipoulizwa iwapo ameshawishiwa au kushinikizwa na watu au ni utashi wake binafsi, Makamba alisema kuwa yote ni mchanganyiko.
“Huwezi kuamka nyumbani na kusema unakwenda kugombea. Kuna msukumo wa wapambe wachache ambao ni lazima ukapime kwa makini kabla ya kuchukua hatua yeyote,” alisema.
“Nchi nzima unakuta inazungumza uwe rais, lazima upime na chagizo hizo ni za kweli au zinatoka wapi. Lakini unaposikia hadi viongozi wa dini, wanafunzi wa vyuo unapokwenda wanakuuliza jambo hilo hilo, unatakiwa utafakari.”
Aliongeza: “Mfano unakwenda Maswa (Shinyanga), Liwale (Lindi), Simanjiro (Kilimanjaro), Wete (Pemba) unaambiwa unafaa, ni muhimu katika hili lakini pia wazee, vijana, viongozi wa dini wanasema unafaa kuwaunganisha Watanzania wote ni jambo la kulitafakari na kulichukulia hatua.”
Februari mwaka huu, Kamati Kuu ya CCM iliwapa onyo kali makada wake sita akiwemo January Makamba ikiwatuhumu kupiga kampeni za urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao kabla ya muda.
Makada wengine waliopewa adhabu hiyo ni mawaziri wakuu wa zamani, Frederick Sumaye na Edward Lowasa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira na mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Pia makamu mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula aliwahi kukemea tabia ya baadhi ya wana-CCM kutangaza mapema nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao, akisema ni wasaliti wakubwa ndani ya chama.

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)