Kurasa

Jumamosi, 14 Juni 2014

WANAWAKE KUPATA RIKIZO YA NGONO KIPINDI HIKI CHA KOMBE LA DUNIA

London, England. Wanawake nchini England na duniani wanajiandaa kwa ajili ya mapumziko ya kimapenzi kutoka kwa waume na wapenzi wao, ambao sasa watazigeukia runinga zao kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Hali ilivyo inaelekea kuwa wasichana watapewa ushirikiano mdogo kuliko ilivyotarajiwa kutokana na wanaume wawili kati ya watano walioulizwa na kukiri kwamba wako radhi kuangalia mpira kuliko kufanya mapenzi.
Kwa mujibu wa uchunguzi, hata kama watakuwa karibu na wapenzi wao, asilimia 42 walisema kuwa watafanya tendo hilo kwa haraka ili kuwahi kuangalia mechi muhimu.
Lakini bado kuna chumba cha makubaliano, baada ya watu zaidi ya asilimia 37, walikubali kuwa wanaweza kukubali ofa ya kufanya mapenzi na wenzi wao kama tu watawekewa runinga kufuatiilia mchezo husika wakati huo.
Zaidi ya nusu walidai kuwa watafikiria zaidi kuangalia mechi nzuri kuliko kwenda kufanya mapenzi na wenzi wao.
Katika msimu huu wa Kombe la Dunia, uhusiano kati ya mapenzi na soka yako wazi, kuna mapenzi ya dhati na mchezo, burudani ya kipekee, lakini kwa wale waliokaa kimya kutozungumzia hali hiyo wanatajwa kuwa kama ‘waigizaji’.
Wakati michuano hiyo ikitarajiwa kutoa burudani ya kutosha uwanjani, majadiliano juu ya majeruhi yamekuwa yakichukua nafasi sambamba na michezo ya kujiangusha.
Hata hivyo, kila mchezaji anayetaka kufanya hivyo anatakiwa kufikiria mara mbili kwa sababu karibu asilimia 70 ya mashabiki wa mpira wanakubaliana kuwa wachezaji wote wanaofanya vituko hivyo uwanjani wanaharibu hali ya utazamaji ya kila mpenda soka.
Mmoja kati ya watatu walioulizwa kuhusu suala hilo alisema ni tukio baya zaidi uwanjani kuliko kulifanya kitandani. Uchunguzi unaonyesha kuwa wengi wao wanakubaliana na uongo wa kukimbia kufanya mapenzi kuliko kufanya uongo uwanjani kwa ajili ya matokeo.
Wanasema wanaweza kusingizia chochote kwa kuumwa, kuwa katika hali mbaya, ili mradi kunakuwa na sababu mbili hadi tatu, utasikia ‘kichwa kinaniuma’, ‘nimefanya kazi kutwa nzima bila kupumzika’, ili mradi kuwe na sababu ya kuangalia mpira.
Watu 2,000 kutoka katika asilimia 72 walikiri kuwa kuna tatizo kubwa katika uhusiano, huku wakionesha jinsi kampeni yao ya kuhamasisha uhusiano mwema iitwayo #DontFakeIt itakavyokuwa katika wakati mgumu.
Msemaji wa kampeni hiyo alisema: “Kuna aina fulani ya wanawake ambao wanajua jinsi ya kuomba udhuru, lakini kipindi cha soka kinapoanza, hali hubadilika.
MWANANCHI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni