Kurasa

Ijumaa, 13 Juni 2014

MWANAMKE AJIFUNGUA MJUSI BAADA YA UJAUZITO WA MIEZI TISA

Mwanamke mmoja nchini Indonesia amejifungua mjusi badala ya mtoto.
Mwanamke huyo Debi Nubatonis, mwenye umri wa miaka 31, ameanza kupata vitisho kutoka kwa kundi la vijana kutokana na kitendo hicho wakimtuhumu kwa uchawi ambapo sasa mamlaka za nchi hiyo zimetuma timu ya wataalamu kwa ajili ya kumaliza utata wa tukio hilo lisilo la kawaida.
Wanasayansi katika timu inayofanya uchunguzi kwa mwanamke huyo wamesema wanahitaji kupatiwa muda wa kutosha kuchunguza tukio hilo na kuja na maelezo ya kueleweka.
Kitendo hicho cha mwanamke kujifungua mjusi badala ya mtoto kilibainishwa na mkunga anayedai kwenda nyumbani kwa mwanamama huyo kumsaidia kujifungua katika kijiji cha Oenunto kwakuwa alishindwa kufika hospitalini.
Madai ya mwanamke huyo kujifungua mjusi yameibua vitisho dhidi ya mwanamke huyo na familia yake ambao wanatuhumiwa kwa uchawi na kuamsha mjadala mkubwa katika mitandao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni