Kurasa

Jumatatu, 19 Mei 2014

RAIS WA BOLVIA ASAJILIWA KUCHEZA SOKA,ATALIPWA 340800.

Hebu tafakari rais wa nchi kuchezea klabu ya kandanda inayoshiriki ligi ya taifa ya daraja la kwanza ?Klabu moja huko Bolivia (Sport Boys) imemsajili rais wa Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo cha kati kuanzia Agosti mwaka huu.
Rais Morales atalipwa mshahara wa dola $213 kwa mwezi .
Morales atavalia jezi nambari 10 katika klabu hiyo iliyoko Kusini mwa Bolivia katika jimbo la Santa Cruz.
Mashabiki wanamsubiri kwa udi na uvumba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni shabiki sugu wa kandanda kushuka dimbani.
Hii kweli Mussa Likudaz umetukomoa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni