Kurasa

Jumanne, 13 Mei 2014

MSIGWA AMLIPUA NYARANDU BUNGENI.


Msemaji mkuu wa kambi ya upinzani Mh.Pita Msigwa amemtuhumu Waziri wa Maliasili na utalii mh.Nyarandu kuwa amemtimua mkurugenzi mkuu wa wizara hiyo na kumteua mtu ambae amehusika katika oparesheni tokomeza ambayo ilikuwa na kashfa ya unyanyasaji mkubwa wa wananchi na kupelekea mawaziri wanne wa wizara mbalimbali ikiwemo ya ulinzi na Maliasili na utaliikuwajibishwa.
Msigwa alisema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya kambi ya upinzani katika uwasilishaji wa hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi ya wizara ya maliasili na utalii bungeni Dodoma jioni ya leo.
Pamoja na hayo, pia Msigwa alizituhumu kampuni mbalimbali zinazojihusisha na maswala ya utalii na uwindaji kuwa ndio yamekuwa yakufanya ujangiri wa hali ya juu kwa wanyama katika mbuga mbalimbali nchini na hivyo kuongoza katika uvunjifu wa sheria za nchi.
Katika kukazia hilo Mh.Msigwa aliweka CD mezani yenye ushahidi wa jinsi moja kati ya kampuni za uwindaji, zinavyokiuka sheria za uwindaji kwa wanyama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni