Kurasa

Jumatatu, 12 Mei 2014

KOPA ASEMA BELLE NINE NDIO MWANAMUZIKI BORA:ATAJA UVUNDO WA KILLI.

MALIKIA wa mipasho nchini, Khadija Kopa ‘Top In Town’, ameponda tuzo za muziki za Kilimanjaro msimu huu, kwa madai kuna watu hawakustahili kupata, huku wakiwaacha wale wenye uwezo mkubwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Kopa alisema hayasemi hayo kutokana na yeye kutopata tuzo, ila alishangazwa na tuzo ya mtunzi bora wa nyimbo, aliyopewa Nassib Abdul ‘Diamond’ huku akinyimwa Abelinego Damiani ‘Belle 9’.
Malikia Kopa alisema yeye binafsi pia hajawahi kuona msanii kokote duniani anapata tuzo saba wakati kuna wenzake wengi, huku akihoji sababu za Diamond kupata tuzo zote hizo huku muandaaji wake wa muziki akikosa tuzo hata moja.
“Diamond kapata tuzo zote hizo, lakini ‘producer’ wake hajapata tuzo, hapo inakuingia akilini? Na hata tuzo ya mtunzi wa taarabu, watu ukumbini walisema Abuu, lakini akapewa mwingine, hilo ni tatizo waliangalie tena katika mashindano yajayo,” alisema na kuongeza kuwa yeye hana kinyongo kukosa tuzo, ila hastaili kuchanganywa na waimbaji watoto, inatakiwa iwepo tuzo ya wakongwe kama yeye na akina Mwanahawa.
Alisema kila akikaa na kusikiliza nyimbo za Belle 9, huwa anafarijika mno na kujiuliza kijana huyo maneno ya kuimba anayatoa wapi, lakini tuzo kanyimwa, inasikitisha.
Aliongeza kuwa kinachomshangaza, mwaka jana wao waliposhinda walitembelea mikoani kufanya ‘tour’, lakini mwaka huu hayumo kwenye tuzo, lakini wanamfuata kumtaka aende mikoani.
“Mimi sio mshindi, lakini nafuatwa kutokana na ubora wangu, mwaka jana tulienda peke yetu mikoani na tukafanya vema, hivyo basi na hawa waende wakafanye wao kama sisi tulivyofanya mwaka jana, lakini nimezungumza nao na tukikubaliana nitaenda,” alisema Kopa.
VIA:TANZANIA DAIMA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni