Kurasa

Jumamosi, 19 Aprili 2014

YANGA BADO HAIJAPATA DAWA YA SIMBA CHEKI MATOKEO YA MECHI HAPA!

Mechi ya Simba na Yanga iliyokua ikichezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam imekamilika kwa sare ya 1-1 huu ni mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,goli la Yanga lilifungwa na Simon msuva dakika ya 86 upande wa Simba ilipata goli dakika ya 75 kupitia Haroun Chanongo.
Uwanja wa Azam Complex Chamazi goli alilofunga Brian Umony limeipa Azam ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu,Azam imemaliza Ligi Kuu na pointi 62 wakati Yanga imemaliza na pointi 56 ambayo imewafanya kushika nafasi ya pili hivyo kuwafanya Azam FC kuwa mabingwa wa Ligi Kuu 2013/2014.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni