Kurasa

Jumamosi, 19 Aprili 2014

BORA POSHO WALE WAATHIRIKA WA MAFURIKO.

Dodoma. Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu la Katiba imepitisha utaratibu ambao kila mjumbe atachangia posho ya siku moja kwa ajili ya kuchangia wahanga wa mafuriko.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan aliliambia Bunge mjini hapa jana kuwa kwa hesabu za posho ya kikao ya Sh70,000, kiasi cha Sh44 milioni kitapatikana.
“Kamati ya Uongozi imekaa na kuafiki wajumbe wote tukatwe posho ya Sh70,000 kwa kila mjumbe kama tulivyoombwa ili ziende kusaidia juhudi za Serikali kusaidia wahanga wa mafurikio,” alisema.
Pendekezo la wajumbe kukatwa posho ya siku kwa kila mjumbe lilitolewa Jumatatu wiki hii na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya.
“Naomba tutoe mchango wa posho ya siku moja itaonyesha hatuko kisiwani na tunaungana na waliopata maafa haya,” alikaririwa Profesa Mwandosya.
Mwandosya aliongeza: “Maana yake ni kwamba Bunge lako tukufu linaweza kuchangia hakika kwa siku moja kiasi ambacho kwa hesabu za haraka haraka haipungui kiasi cha Sh180 milioni,” alisema.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta alisema pendekezo hilo lingepelekwa kwenye Kamati ya Uongozi na kujadiliwa.
Hab

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni