Kurasa

Jumamosi, 19 Aprili 2014

SITTA AHAHA KUWARUDISHA UKAWA BUNGENI.

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta anahaha kulinusuru Bunge hilo, baada ya wajumbe ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao vinavyoendelea mjini Dodoma.
Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zilisema Sitta anawasaka viongozi wa Ukawa kwa lengo la kukaa nao katika meza ya mazungumzo, kutafuta maridhiano yatakayowezesha kundi hilo kurejea bungeni.
Sitta jana aliliambia Mwananchi kuwa wako njiapanda, kwa sababu hawafahamu kama wajumbe hao wa Ukawa wametoka tu nje ya ukumbi na watarudi au wamejiuzulu. (P.T)
KUTOKA MWANANCHI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni