Kurasa

Jumamosi, 19 Aprili 2014

POLISI WADAIWA KUUA MTU!HEBU SOMA HAPA

Serengeti. Utata umegubika mazingira ya kifo cha Emmanuel Mtongori (20), mkazi wa Kijiji cha Rung’abure, wilayani Serengeti inayedaiwa kupigwa risasi eneo la Mgodi wa African Barrick North Mara na kufariki dunia akiwa Kituo cha Polisi Nyamongo.
Hatua hiyo inatokana na taarifa za ndugu wa marehemu akiwamo baba yake mzazi, Mtongori Nyagwisi kudai kabla ya kijana wake hajafa alimwambia alipigwa risasi na polisi. Hata hivyo, Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime/Rorya, Justus Kamugisha alikanusha madai hayo na kusema kwamba, walimwokota kijana huyo baada ya kupigwa risasi na majambazi.
Akizungumza kwa simu juzi, Nyangwisi alidai Aprili 15 mwaka huu saa 5:30 asubuhi, alipigiwa simu na polisi wa Kituo cha Nyamongo, wilayani Tarime na kumtaarifu kuwa kijana wake ana hali mbaya na amelazwa Hospitali ya Sungusungu Nyamongo.
“Aprili 16 nililazimika kwenda kumwona… nikamkuta Hospitali ya Sungusungu Nyamongo akiwa amelazwa hapo akanieleza mazingira yaliyomkuta kuwa alipigwa risasi na polisi baada ya kumwamuru asimame akitokea eneo la mgodi,” alidai Nyangwisi na kuongeza:
“Alikimbia na kupigwa risasi kiunoni akaanguka, wakamchukua na kumweka ndani ya gari, polisi walipoona hali siyo nzuri wakampeleka hospitalini na kumtaka awatajie namba ya mtu anayemfahamu akawapa namba yangu ndipo wakanipigia.”
Alidai akiwa anaongea naye, polisi walimtaka kuondoka na kwamba, haruhusiwi kumhudumia kwa sababu akipona watamshtaki kwa kuvamia mgodi.
Nyangwisi alidai licha ya kijana wake kuwa na hali mbaya, polisi walimtoa hospitalini hadi kituo cha Nyamongo kwa madai kuwa wanachukua maelezo yake tangu saa 2:00 hadi 5:00 asubuhi alipofariki dunia.
Adaiwa kuporwa simu:
Baada ya kubainika amekufa, Nyangwisi akiwa anapiga simu kwa ndugu zake, polisi wanadaiwa walimnyang’anya simu kwa madai anawapigia kelele na kupeleka maiti Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
“Pale hospitali polisi walifika na kunichukua hadi ofisi zao, lakini nililazimika kumwona RPC (Kamanda wa Polisi Mkoa) nikamsimulia kisa chote hakuwa na taarifa… akaamuru nirudishiwe simu yangu,” alisema.
Akutwa golori za risasi nane
Kwa mujibu wa Nyangwisi, Imori Sinda na Stephen Giboma walioshuhudia uchunguzi wa mwili, golori nane zilikutwa tumboni ambazo alipigwa kwa nyuma, huku askari wakibishana wao kwa wao.
KUTOKA MWANANCHI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni