Kurasa

Jumatano, 23 Aprili 2014

MASKINI HUYU JAMAA!YANI CHARGER YA SIMU TU IMEMUUA.

FUNDI magari, Mohamed Athuman (52), mkazi wa maeneo ya Wandengereko, Mtoni-Mtongani, Dar es Salaam, amefariki dunia juzi kutokana na hitilafu ya umeme katika waya wa chaji ya simu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3 asubuhi wakati Athuman alipokuwa akichomeka chaji hiyo katika soketi ya ukutani.
Alisema Athumani alifariki dunia papo hapo na maiti imehifadhiwa Hospitali ya Temeke.
Katika tukio jingine, maiti ya mtu aliyetambuliwa kwa jina la Jamal Hamis (20) mfanyabiashara, mkazi wa Yombo Dovya imekutwa ufukweni mwa Bahari ya Hindi, eneo la Mtoni Kijichi.
Kamanda Kiondo alisema maiti hiyo ilikutwa juzi, saa 6 mchana ikiwa inaelea ndani ya maji.
Alisema Aprili 21, majira ya jioni, Athumani alikuwa akiogelea na mwenzake Said Salum na ndipo ghafla wote walizidiwa na kuzama ndani ya maji.
Hata hivyo mwenzake aliokolewa na wananchi wa eneo hilo na yeye hakuonekana hadi ilipokutwa maiti yake. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Temeke.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni