Kurasa

Jumatano, 23 Aprili 2014

HE!KUMBE WALIMU WANATAKA SERIKALI TATU!!

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimesisitiza kuwa msimamo wa chama hicho ni muundo wa serikali tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema chama hicho mwishoni mwa mwaka jana kikiwa taasisi huru kilikaa kama Baraza la Katiba na kuazimia juu ya muundo wa Muungano wa serikali tatu.
Alisema baada ya Mkutano Mkuu kupitisha kwa kauli moja hoja hiyo Oktoba alipeleka maoni yao kwenye ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuyakabidhi.
“Tuliposikia rasimu ya pili imetoa maoni hayo tuliridhika kuwa maoni yetu yamekubalika,” alisema Mukoba.
Aidha, Mukoba alisema CWT kama zilivyo taasisi nyingine kina wanachama wengi wenye mitizamo tofauti, lakini kikifikia makubaliano katika mambo ya msingi lazima maoni ya taasisi yawekwe mbele, na maoni binafsi yahifadhiwe moyoni.
“Juzi tukiwa Tanga kwenye Baraza la CWT lililokaa Aprili 15-16 Aprili, 2014 wajumbe walisisitiza msimamo wao juu ya muundo wa serikali tatu na kuniagiza niongee na vyombo vya habari ili kuuweka wazi.
“Kwa kuwa mimi ndiye msemaji wa CWT, narudia tena kusema msimamo wetu ni muundo wa Muungano wa serikali tatu,” alisema.KUTOKA TANZANIA DAIMA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni