Kurasa

Alhamisi, 17 Aprili 2014

KESI YA PINDA YAPIGWA TAREHE.

Thursday, April 17, 2014

MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepiga kalenda kutoa uamuzi wa kesi ya kikatiba dhidi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hadi Mei 19 mwaka huu, itakapotoa uamuzi wa pingamizi la awali lililowasilishwa na upande wa Jamhuri.
Uamuzi huo ulipangwa kutolewa jana lakini iliahirishwa mbele ya Msajiri Benedicto Mwingwa baada ya jopo linalosikiliza kesi hiyo kuwa bado halijamaliza kuandika uamuzi huo.
Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji waatu likiongozwa na mwenyekiti wao Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu.
Kesi hiyo Namba 24 ya 2013 ilifunguliwa na Kituo Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
LHRC na TLS,wanadai Pinda alivunja Katiba kutokana na kauli aliyowahi kuitoa bungeni wakidai kuwa ni amri kwa vyombo vya utekelezaji wa Sheria kuwapiga wananchi, wakati wa vurugu. Hivyo wanaiomba mahakama, pamoja na mambo mengine, itamke kuwa kauli hiyo ni kinyume cha Katiba na imwamuru Pinda aifute hadharani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni