Kurasa

Jumamosi, 26 Aprili 2014

INAKUWAJE UNASABABISHA KIFO CHA MMEO.

Mbaroni kwa kumuua mumewe
MKAZI wa Kata ya Kisemvule, Tarafa ya Vikindu, wilayani Mkuranga, Husna Kisoma (16), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kusababisha mauaji ya mumewe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amemtaja marehemu kuwa ni Jumanne Mwarami (21).
Tukio hilo limetokea juzi usiku na linadaiwa kusababishwa na wivu wa mapenzi baada ya marehemu kuibua ugomvi kati yake na mkewe akimtuhumu kuwa si muaminifu katika ndoa yao.
Katika ugomvi huo Husna alimvuta mumewe sehemu zake za siri, hali iliyosababisha kupoteza maisha alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni