Kurasa

Jumatatu, 27 Januari 2014

ZAWADI/ GIFT

YALIYOMO

SHUKURANI……………………………………………………………………………………………………………………..I
UTANGULIZI……………………………………………………………………………………………………………………..II
DIBAJI………………………………………………………………………………………………………………………………..III





















SHUKURANI
Sitakuwa nimefanya lolote kama nisipoanza kumshukuru MWENYE ENZI MUNGU muweza wa yote ambae ameniwezesha kuwa miongoni mwa watu ambao ameamua waendelee kuishi katika hii dunia .Pamoja na kuniwezesha kuishi pia ameendelea kunisimamia katika mamba mbalimbali yanayohusiana na maisha yangu hapa duniani katika halinzuri na hali mbaya .Nashukuru kwa yote kwa kuwa mambo hayo ndio yanayofanya maisha yaitwe maisha na kila iakimoja kinasababu maalum ya kuwepo katika nafasi yake kwa hiyo kila linalotokea tunapaswa kushukuru.
Shukurani nyingine za dhati kabisa ni kwa mke wangu mpendwa ambae amekuwa na mimi bega kwa bega katika hali zote zinazohusiana na maisha.Namshukuru kwa upole na moyowake wa uvumilivupamoja na mzigo wate wa majukumu aliyonayo ya kuitunza familia.
Pamoja na wote hao nawashukuru wazazi wangu walionizaa akiwemo mama yangu mpendwa ambae sasa ametangulia mbele ya haki,Baba yangu mzee Mukebezi ambae Mungu anaendelea kumpa moyo wa subira kwa kumpoteza mke wake mpenzi,ndugu jamaa na marafiki zangu wate akiwemo kaka yangu mpendwa ambae amekuwa akinisimamia sana kwa hali na mali kw ayote ninayoyafanya.












UTANGULIZI
Hadithi hii inatokana na ukweli uliopo kwenye maisha yetu ya kila siku.Watu wengi wamekuwa wakikata tamaa katika maisha na hasa wanafunzi mashuleni kwa kisingizio kuwa maisha yao ni duni hivyo hata wakijitahidi hawawezi kufanikiwa katika maisha.Mawazo hayo ni potofu kwa kuwa hakuna binadamu yoyote aliezaliwa na pesa isipokuwa ni juhudi na maarifa za baadhi ya binadamu ndio zinazowafanya kuitwa mamilionea,mabilionea au hata kuwa na nafasi ambazo wamekuwa wakiota kuwa nazo katika maisha.
Msichana JENI ambae baadae alib adilishwa jina kuwa ZAWADI ni kiwakilishi tu cha watu ambao pamoja na yote yaliyotokea katika maisha hawakati tama na wanaendelea kupambana mpaka mwisho wa siku wanafanikiwa kupata kile wanachokusudiwa kukipata.
Pamoja na kufiwa na wazazi wake wote tena kwa kuliwa na wanyama wakali wa majini aina ya mamba Jeni chini ya mikono ya mwanamke msamalia anafanikiwa kupambana na vikwazo vyote vya maisha mpaka kufanikiwa kuwa na cheo kikubwa kabisa katika nchi ingawa kazi hiyo haikuwa rahisi.Endelea kuisoma hadithi hii ujue ni jinsi gani msichana jasiri ZAWADI ataweza kutimiza malengo yake.

MUKEBEZI,Deonidas G(2014)Muandishi wa habari
A journalist &teacher.

















MOJA 1
Walitembea kwa uangalifu kila mmoja akiwa makini kuangalia eneo zuri ambalo litafanana au litakaribia kufanana na eneo la mwanzo.Akiwa na mawazo mengi juu ya ya umaskini uliokithiri katika familia yake,juu ya jinsi ambavyo motto wake wa kike atakavyoishi bila matatizo ambae kwa wakati huo alikuwa ndio kwanza ana umli wa mwaka mmoja,Pia akiwaza kuhusiana na jinsi ya kuwakwepa polisi ambao ndio walikuwa kikwazo kikubwa katika biashara yao,mzee John aliweza kuona mto mkubwa ambao ulikuwa na maji yaliyokuwa yanateremka taratiibu kuelekea bondeni.
Alimshika mkono mke wake mama Jeni ambae wakati huo alikuwa amembeba Jeni mgongani,wakasogea karibu kabisa na mto huo ambao ulionekana kuwa mkubwa kuliko mto wa mwanzo.
Wiki moja iliyopita mzee john na wenzake walitimuliwa kutoka katika eneo lao ambalo walizoea kutengeneza pombe haramu aina ya chang’aa(gongo) na maafisa wa polisi,ambao walipewa habari ya kuwepo kwa eneo hilo na raia ambae alipita katika harakati zake na kugundua maficho hayo amayo yalikuwa na mitambo na mapipa mengi kwaajili ya kazi maalum ya kuchemsha gongo.
“Nafikiri hapa panafaa”alisema mzee John
“Sana!tena pamejificha kuliko eneo la mwanzo”mama Jeni alimuunga mkono mumewe.
Mzee John aliendelea kukagua eneo zuri ambalo lingefaa zaidi kwa kazi yao kando yam to huo.Wakati huo mama Jeni aliamua kusoge karibu na maji ili amsafishe Jeni ambae alianza kulia kwa kwa sauti kutokana na mkojo ambao ulilowanisha nguo na za mama yake.
Mama Jeni alifungua kanga ambayo aliifunga kwa utaalamu wa asili ili kumfanya motto asidondoke kutoka mgongoni,na kumshusha Jeni ambae kwa wakati huo alionekana kufurahia kutokana na kuhisi kuwa kilio chake kimesikiwa.Akiwa katika harakati za kumsafisha Jeni mala ghafla bila kutegemea aliona kitu kama kifaa cha kuchania mbao aina ya msumeno kikiubana mguu wake wa kushoto.Kabla hajatafakari dubwana lile lilianza kumvuta mzimamzima kuelekea mtoni.
“Mama weeee”

Baba Jeni aliisikia sauti ya mkewe akiwa tayari yuko mbali sana na eneo la tukio.Alijitahidi kuiamlisha miguu yake imbibe kadiri inavyoweza kuelekea mahali walipokuwa mama Jeni na motto wao Jeni.Akiwa bado yuko mbali aliweza kumuona mkeweambae alikuwa amemkumbatia motto wake Jeni kw makini sana akipambana bila mafanikio kujitoa katika ya wanyama wale ambao sasa walikuwa wawili na ambao walikuwa hawapo tayari kuliachia windo lao asubuhi ile.
Mzee John alifika na kumchukua Jeni ambae alimlaza pembeni yam to ule mbali kidogo na eneo lile.Ilikuwa kama Jeni ndio alikuwa anaongeza uzito na moyo wa kupambana kwa mama yake kwani baada ya kuondolewa kwenye mikono ya mama yake,mama Jeni nguvu zilimuishia na ikawa rahisi kwa mamba wawili wakubwa kumvutia mama Jeni mtoni.
Wakati mzee Joni anafika eneo lile ili aweze kumsaidia mke wake, alishuhudia kichwa cha mkewe kikitokeza kwenye maji ghafla na kupotea moja kwa moja.Bila kutafakari mzee John alijitosa kwenye maji ili kumtafuta mkewe.Kwa bahati mbaya mzee John hakufahamu kina cha mto ule na hakuwa na ujuzi wowote wa kuogelea.Kutokana na ukweli huo mzee John alipoingia tumoja kwa moja alijikuta anamezwa na maji ambayo hakuweza kupambana nayo.
Maji yale yalimtoa nje mala ya kwanza na mala ya pili,mala ya tatu alishukia kwenye midomo ya mamba ambao waligombania supu na minofu ya mwili wa mzee kama wana njaa ya siku tano.Mto ulibadilika na kuwa na rangi nyekundu na eneo lote lilitoa harufu ya damu.
Mtoto Jeni baada ya kusubili kwa muda,uvumilivu ulimshinda na akaanza kulia kwa sauti kali bila mafanikio.Kwa muda wa nusu saa nzima Jeni alilia mpaka sauti ilikuwa hafifu na mwisho akapitiwa na usingizi na kulala…
























MBILI 2
Bi Zainabu ambae alikuwa hana mume wala mtoto na ambae alimua kuishi maisha ya upweke msituni kutokana na matatizo ambayo alishakumbana nayo zamani,alikuwa akipitappita msituni kujiokotea kuni kwaajili ya kwenda kujipikia chakula baada ya kazi nzito. ya kulima kijishamba kidogo kilichokuwa nyuma ya kibanda chake.Hakuwa na wazo lolote juu ya atakachokiona kule alikokuwa anaelekea zaidi ya kuni.Ghafla kwa mbali aliweza kuoona kitu kama jiwe limelala kando yam to.Aliposogea zaidi alishangaa kuona mtoto mzuri mwenye afya amelala usingizi mzito.Alihisi kuwa mtoto huyo alikuwa ni mmoja kati ya watoto wa kijiji cha BOMA ambacho kipo karibu kabisa na mahali hapo alipokuwaanashi peke yake.
Mawazo mengi yalimjia kwa wakati mmoja na hakujua aanze na lipi.Aina ya maisha aliyokuwa anaishi ilikuwa ni kutokana na ukweli kuwa hakuwahi ku bahatika kupata mtoto katika maisha yake.Je!mtoto huyo alikuwa ni zawadi kutoka kwa mungu?,Au je ampeleke motto huyu kwa mwenyekiti wa kijiji na kuitupa zawadi hiyo?Kama sivyo je!amuache motto huyo mahali alipo?Mtoto Yule alikuwa ni mtu au ni shetani?Nani kamuweka mahali pale?....Kwanini?..........?.............?....................?.....................?.Maswali mengi yalikuja kichwani kwake kama umeme na hakujua aamue lipi aache lipi
Bi Zainabu alimuinamia na kumbeba mtoto kwa uangalifu mkubwa asimuamshe kutoka katika usingizi.Alimpenda sana motto Yule na kwa upendo huo tayari bi Zainabu alishapata jibu la maswali mengi yaliyokuwa yanamsumbua…
Aliamua kuacha shughuli ya kutafuta kuni na kumpeleka motto nyumabani kwake ambapo alimtengenezea mahali pazuri pa kulala.Baada ya kumlaza motto na kuhalilisha kuwa yuko salama na amelala usingizi,bi Zainabu aliwasha moto na kumtengenezea uji mtoto Yule.
Baada ya nusu saa uji ulikuwa tayari na Bi Zainabu alimuamsha mtoto na kuanza kumlisha uji ambao aliunywa bila kipingamizi kutokana na njaa aliyokuwa nayo.Wakati wote huo bi Zainabu alikuwa akiwaza kwa furaha jinsi Mungu alivyosikia kilio chake na kumpatia motto.
Zamani alipokuwa mwanafunzi kila mwanaume alitamanni kumuoa kutokana na uzuri wake wa umbo na sura.Baada ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi pango Zainabu alichumbiwa na kijana mtanashati kutoka jijini Dar es salaam na siku zilipotimia aliolew na kuhamia jijini Dar es salaam kwa kijana Zuberi.
Kwa mwaka mzima Zuberi na Zainabu waliishi maisha ya furaha na amani wakifanya starehe za kila aina kutokana na ukwli kuwa Zuberi alikuwa anajiweza kiuchumi.Baadaya muda kupita Zuberi alianza kubadilika hasa baada ya kugundua kuwa muda mrefu ulipita bila ya Zainabu kushika ujauzito.Zuberi alianza kuchelewa kurudi nyumbani na hata alipokuwa anarudi mapema Zainabu aliambullia kipigo na matuisi.Zainabu alivumilia hali hiyo kwa muda wa miaka miwili na hatimae uzalendo ukamshinda na akaamua kurudi nyumbani kijijini Pango na kuendelea kuishi na wazazi wake kama mwanzo.
Kama wahenga wasemavyo ukisema cha nini wenzako wanawaza watakipata lini,baada ya miezi sita Zainabu aliolewa tena na mwanaume mwenye maisha ya kawaida kutokajijini Mwanza.Waliishi maisha ya upendo kama mke na mume,lakini baada ya miezi nane tumwanaume Yule hakuwa tayari kuvumilia zaidi na akaamua kumuacha Zainabu kwa kigezo kile kile cha kutokupata mtoto.Zainabu aliapa kutokuolewa tena nje ya kijiji chao.Alikaa miaka mitatu,kipindi hicho akiwa na umli wa miaka ishirini na nne na kupata mwanaume mwingine kutoka kijijini kwao Pango kama alivyo taka ambae alikuwa maskini kama yeye.Zainabu aliishi kwa rah asana na mwanume huyo kutokana na kumueleza mwanaume huyo ukweli wote kabla hata hawajaoana na akakubaliana na hali ya Zainabu ya kuto kushika ujauzito.Pia Zainabu alimueleza mwanaume huyo yote yaliyo mpata katika maisha yake yaliyopita na mwanaume huyo akamuahidi kuwa hatamuacha na ataishi nae mpaka kifo kitakapowatenganisha.
Zainabu aliishi na mwanaume huyo kwa muda wa miaka mitano na alionekana kumpenda sana bila kujali hali yake.Zainabu alijihisi yulo salama sana katika mikono ya Hamisi ambae alimuona kama ni zawadi kutoka kwa Mungu.Kazi yake kubwa aliyokuwa anafanya Hamisi ilikuwa kilimo cha maharagwe na mahindi.Kila asubuhi Hamisi na mkewe walikuwa wanaelekea shambani kwaajili ya kuendelea kufanya shughuli zao za kawaida za kilimo.
Ilikuwa ni siku ya jumatano,siku ambayo ilibadilisha kabisa maisha ya Zainabu na ni siku ambayo Zainabu hawezi kuisahau katika maisha yake.Wakiwa wametoka asubuhi kwa furaha kabisa na mume wake,na siku hiyo jua likiwa ni la wastani,wanandoa hao walipanga kuitumia siku hiyo kuchoma mabiwi kwaajili ya kupanda mbegu.Walifika mapema kabisa shamban na kuanza kazi mala moja.Hamisi aliamua kuyakusanya mabiwi kwa wingi ili ayachome kwa pamoja.Aliyasogeza mabiwi hayo karibu kabisa na mpaka ws shamba la jilani ambalo lilikuwa na miwa mingi yenye majani makvu.Bila kufikiri Hamisi alimuagiza kibiriti mkewe na kuyawasha moto mabiwi mengi sana aliyoyakusanya.
Mabiwi yale yalianza kuwaka taratibu lakini baada ya muda mfupi moto ule ulikuwa mkali na wa kutisha.Kabla hajakaa sawa moto ulikamata majani makavu yaliyokuwa kwenye shamba la jilani na kuanza kutembea kuelekea kwenye miwa ya jilani.Hamisi hakuwa na jinsi alishaiona hatari ambayo ingetokea mbeleni.Alijaribu kuuzima moto ule kwa kutumia majani ya miti lakini haikusaidia.Kwakuwa katika shamba la jirani kulikuwa na kijoto kidogo kilichokuwa kinatiriririka,aliamua kuuzima moto ule kwa kutumia maji.Maji hayakusaidia kutokana na ukavu wa majani na umbali kutoka mahali ambapo moto ulikuwa unawaka na mtoni na hivyo moto uliendelea kuwa mkali zaidi ya mwanzo.
Kwa kipindi ambacho alikuwa anahangaika kuuzima moto ule,Hamisi alitumia muda mrefu sana kiasi kwamba moto ulifika karibu kabisa na shamba la miwa la jirani yake.Aligundua kuwa hakuwa na muda tena wa kulima njia kuzuia moto usipite kuelekea kwenye miwa hiyo.Alitumia muda wa sekunde kadhaa kuwaza njia ya haraka ambayo ingemsaidia kupata suluhisho la halaka na ndipo alipokumbuka moja ya misemo ya zamani kabisa ‘Dawa ya moto nimoto’.Hilo ndilo tumaini pekee alilokuwa nalo Hamisi kwa wakati huo kwa kuwa njia zote zilishindwa.Alikumbuka siku moja wakati yuko darasa la tano mwalimu wao wa Kiswahili aliwaeleza kuwa moto unapokuwa mkubwa katika eneo lililowazi,ukiwasha moto mwingine mbele yake utavutwa kuelekea kwenye moto huo mkubwa.
Hamisi alijaribu!.Alichukua kibiriti na kuwasha moto mwingine mbele kidogo ya moto ule mkubwa ambao sasa ulikuwa unaunguruma na kutoa miali ya kutisha kama radi wakati wa msimu wa vuli.Haikuchukua muda moto mdogo aliouwsha Hamisi ulianza kushika kasi na kuwa mkubwa.Moto huo ulianza kuvutwa kuelekea ulipokuwa moto ule mkubwa uliokuwa ukiendelea kuunguruma kwa msaada wa upepo.Kutokana na hali hiyo moto mkubwa ulianza kuzunguuka na kutengeneza alama ya mwezi mchanga.Kutokana na kuchanganyikiwa Hamisi alisahau kuwa aliwasha moto mdogo akiwa yuko katikati,na alibaki anashangaa moto ule aliowasha ulivyokuwa unavutwa kwa nguvu na moto mkubwa na kufurahi moyoni kuwa amefanikiwa jaribio lake.
“Hamisiiiiiiiii” Alisikia sauti ya mkewe ikimuita na alipostuka akajikuta yuko katikati ya moto uliomzunguka pande zote.Moto ulikuwa mkubwa kiasi kwamba hakuweza kuona kundi kubwa la wanaume wa kijijini Pango walifuatana na Zainabu kwenda kumsaidia mumewe baada ya Zainabu kwenda kuomba msaada.Walijitahidi kuuzima moto ule,lakini kwa muda waliofika walishachelewa sana.Moshi ulikuwa mwingi sana kiasi cha kufanya Hamisi ashindwe hata kutoa sauti.Pumzi zilimuishia na akadondoka chini.Moto mdogo na ule mkubwa viliweza kuungana kabisa Hamisi akiwa katikati.Huo ukawa ndio mwisho wa mume kipenzi wa Zainabu,Hamisi.
Moto ulipopungua wanakijiji waliweza kuuona mwili wa Hamisi ukiwa umeiva na kuwa mwekundu kama mbuzi wa kuchoma(ndafu).Hakuna aliependa kumtazama Hamisi mala mbili!.Wanakijiji waliubeba mwli wa marehemu na kuurudisha kijijini kujiweka tayari kwaajili ya mazishi.Wakati wote huo Zainabu alishazimia na kuzinduka mala mbili nab ado alikuwa hajitambui kw auchungu mkubwa aliokuwa nao wa kuondokewa na mwanaume ambae ...........................USIKOSE KUJUA KILICHOENDELEA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni