Kurasa

Jumatano, 29 Januari 2014

MAHAKAMA YAMUACHIA KIBANDA HURU

Na vitendo issa

Mahakama ya kisutu leo imemwachia huru mhariri mtendaji mkuu wa New Habari (2006), Absalom Kibanda na wenzake wawili, Samsoni Mwigamba, mwandishi wa gazeti la Tanzani Daima na Theophili Makunga meneja uendeshaji biashara wa kampuni ya Mwananchi Communication Limited,dhidi ya kesi iliyokuwa inawakabili.

Kibanda na wenzake walikuwa wanakabiliwa na kesi ya uchochezi dhidi ya askari wa jeshi la ulinzi kwa kuchapisha makala kwenye gazeti la Tanzania Daima yenye maneno yaliyolenga kushawishi kutowatii viongozi wao.

Waandishi mbalimbali walioudhulia kesi hiyo walionyesha kuwa wenye furaha mara baada ya ukumu hiyo kutolewa kutokana na matukio mbalimbali yaliyokuwa yanajitokeza karibuni yanayoashiria kuwa uhuru wa vyombo vya habari hauzingatiwi ipasavyo Tanzania.
PICHA MBALIMBALI ZA KIBANDA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni