Kurasa

Jumatatu, 30 Desemba 2013

TUJILINDE NA KIPINDUPINDU

Nianze kwa kuipongeza sana serikali kwa juhudi zao kubwa ilizozifanya kupunguza kama sio kuondoa kabisa tatizo la kipindupindu ambacho kilikuwa tishio kubwa sana katika baadhi ya maeneo nchini kwetu hususani wakati wa msimu wa matunda aina ya maembe kama huu.

Pamoja na kuipongeza serikali,juhudi zote hizo zingekuwa bure kama wananchi wasingetaka kusikiliza ushauri na maelekezo ya serikali juu ya usafi na kutunza mazingira yanayowazunguuka kwa ujumla.Hii inamaanisha kuwa pamoja na kuwa lawama zote tunaitupiaga serikali,mhusika mkuu katika kila kitu anabaki kuwa mwananchi na anaeumia pia ni huyohuyo mwananchi.

Nimeanza kutamka hayo yote kutokana na hali inayoonekana sasa hivi katika baadhi ya maeneo katika nchi yetu,ambayo inatishia sana kuripuka upya kwa ugonjwa wa kipindupindu kama umakini hautatiliwa maanani.

Baadhi ya masoko ambayo yamekuwa yakifanya biashara ya matunda hayo aina ya maembe yamekuwa yakifanya biashara hiyo bila kuzingatia swala la usafi ambalo ni muhimu sana ili kuendelea kuudhibiti ugonjwa huo usitokee na kuleta madhara ambaya yamewahi kulikumba taifa letu hapo kabla na kusababisha mamia ya watanzania kupoteza maisha yao.

Mfano wa masoko ya matunda aina ya maembe linalotishia mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu,ni soko lililoko KWAMTORO,barabara ya kuelekea Bagamoyo ambalo kimsingi halizingatii kanuni za usafi na kutishia wananchi wanaozunguuka eneo hilo kuingia katika janga la kipindupindu.

Napenda kuwakumbusha watanzania wenzangu kuwa ni vizuri kufanya kosa na kujilekebisha lakini sio vizuri hata kidogo kurudia kosa kwasababu matokeo yake yanaweza kuwa ni makubwa kuliko yale yaliyoonekana mwanzo.

Tujipende wenyewe,tuzipende afya zetu na tuwapende watanzania wenzetu na kuwalinda wasipatwe na magonjwa ambayo sisi tunaweza kuwa ndio chanzo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni