Kurasa

Jumatatu, 30 Desemba 2013

KIKWETE AMKASHIFU LISSU

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr,Jakaya Mlisho Kikwete leo amemkashifu Mbunge na mwanasheria wa CHADEMA mheshimiwa Tundu Lissu kuwa ni mwanasheria lakini amekuwa akizichanganya sheria na hivyo kuwachanganya wale anaowaongoza.

Mheshimiwa Kikwete alitamka hayo alipokuwa anahutubia wananchi na viongozi mbalimbali, katika kikao cha kukabidhi rasimu ya pili ya katiba mpya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania huko Zanzibar leo mchana kilichohudhuliwa na viongozi wengi akiwemo Rais wa Zanzibar mheshimiwa Alli Mohamedi Shein.

Pamoja na hayo Dr,Kikwete pia amewataka watu katika makundi mbalimbali ambao wana nia ya kuwakilisha makundi yao kuwasilisha majina yao mapema ili wasiipoteze fulsa hiyo ya kuwakilisha makundi yao kwa kuwa muda hautoshi.

"Natoa rai kwa makundi mbalimbali ambayo hayajawasilisha majina yao kufanya hivyo mapema ili wasiipoteze fulsa hiyo adhimu ya uwakilishi."alisema Kikwete.

Nae mwenyekiti wa tume ya katiba waziri mkuu mstaafu jaji Josepph Sinde Walioba akizungumzia rasimu hiyo ya katiba alisema kuwa rrasimu hiyo ilikuwa imepunguza sana madaraka ya rais na hivyo itaondoa hofu ya wananchi kuwa rais alikuwa na madaraka makubwa sana.

Kikao hicho kimekamilika leo na rais amewataka viongozi wanaohusika kuitoa rasimu hiyo kwenye mitandao ili kuwafanya wananchi waisome kwa undani zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni