Kurasa

Jumatatu, 30 Desemba 2013

WATANZANIA TUHAMASISHE WATALII WA NNJE KWA KUFANYA UTALII WA NDANI

Ukimuuliza mtanzania wa kawaida leo kama anamfahamu mnyama aina ya mamba atakwambia alimuona kwenye luninga tu na wala hajawahi kumuona moja kwa moja.

Sio kwamba wanyama hao na wengine hawapatikani Tanzania isipokuwa watanzania tumekuwa na utaratibu wa kutokutembelea vivutio vilivyoko kwenye nchi yetu wenyewe na wakati huo huo tukilalamika kuwa serikali haifanyi jitihada za kutosha kuvutia watalii wengi zaidi kutoka nchi za nje na hatimae kuiingizia serikali pesa za kutosha.

Zamani tulikuwa tunatoa sababu mbalimbali kuwa viingilio katika vivuto vya watalii ni vikubwa sana kiasi kwamba tunashindwa kumudu ghalama zake,lakini kwa sasa hatuna sababu yoyote ya kutoa kwa kuwa gharama hizo ziko chini sana na wakati mwingine mtanzania anaweza kutembelea maeneo hayo hata bule.

Hapa najaribu tu kuwaonesha mamba wanaopatikana mji wa Bagamoyo mkoa wa pwani ambao wangekuwa sababu tosha kwa wakazi wa maeneo ya karibu kama Dar es salaam na maeneo ya pembezoni kutembelea eneo hilo na kupata historia zaidi ya mji huo;

TUJILINDE NA KIPINDUPINDU

Nianze kwa kuipongeza sana serikali kwa juhudi zao kubwa ilizozifanya kupunguza kama sio kuondoa kabisa tatizo la kipindupindu ambacho kilikuwa tishio kubwa sana katika baadhi ya maeneo nchini kwetu hususani wakati wa msimu wa matunda aina ya maembe kama huu.

Pamoja na kuipongeza serikali,juhudi zote hizo zingekuwa bure kama wananchi wasingetaka kusikiliza ushauri na maelekezo ya serikali juu ya usafi na kutunza mazingira yanayowazunguuka kwa ujumla.Hii inamaanisha kuwa pamoja na kuwa lawama zote tunaitupiaga serikali,mhusika mkuu katika kila kitu anabaki kuwa mwananchi na anaeumia pia ni huyohuyo mwananchi.

Nimeanza kutamka hayo yote kutokana na hali inayoonekana sasa hivi katika baadhi ya maeneo katika nchi yetu,ambayo inatishia sana kuripuka upya kwa ugonjwa wa kipindupindu kama umakini hautatiliwa maanani.

Baadhi ya masoko ambayo yamekuwa yakifanya biashara ya matunda hayo aina ya maembe yamekuwa yakifanya biashara hiyo bila kuzingatia swala la usafi ambalo ni muhimu sana ili kuendelea kuudhibiti ugonjwa huo usitokee na kuleta madhara ambaya yamewahi kulikumba taifa letu hapo kabla na kusababisha mamia ya watanzania kupoteza maisha yao.

Mfano wa masoko ya matunda aina ya maembe linalotishia mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu,ni soko lililoko KWAMTORO,barabara ya kuelekea Bagamoyo ambalo kimsingi halizingatii kanuni za usafi na kutishia wananchi wanaozunguuka eneo hilo kuingia katika janga la kipindupindu.

Napenda kuwakumbusha watanzania wenzangu kuwa ni vizuri kufanya kosa na kujilekebisha lakini sio vizuri hata kidogo kurudia kosa kwasababu matokeo yake yanaweza kuwa ni makubwa kuliko yale yaliyoonekana mwanzo.

Tujipende wenyewe,tuzipende afya zetu na tuwapende watanzania wenzetu na kuwalinda wasipatwe na magonjwa ambayo sisi tunaweza kuwa ndio chanzo.

KIKWETE AMKASHIFU LISSU

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr,Jakaya Mlisho Kikwete leo amemkashifu Mbunge na mwanasheria wa CHADEMA mheshimiwa Tundu Lissu kuwa ni mwanasheria lakini amekuwa akizichanganya sheria na hivyo kuwachanganya wale anaowaongoza.

Mheshimiwa Kikwete alitamka hayo alipokuwa anahutubia wananchi na viongozi mbalimbali, katika kikao cha kukabidhi rasimu ya pili ya katiba mpya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania huko Zanzibar leo mchana kilichohudhuliwa na viongozi wengi akiwemo Rais wa Zanzibar mheshimiwa Alli Mohamedi Shein.

Pamoja na hayo Dr,Kikwete pia amewataka watu katika makundi mbalimbali ambao wana nia ya kuwakilisha makundi yao kuwasilisha majina yao mapema ili wasiipoteze fulsa hiyo ya kuwakilisha makundi yao kwa kuwa muda hautoshi.

"Natoa rai kwa makundi mbalimbali ambayo hayajawasilisha majina yao kufanya hivyo mapema ili wasiipoteze fulsa hiyo adhimu ya uwakilishi."alisema Kikwete.

Nae mwenyekiti wa tume ya katiba waziri mkuu mstaafu jaji Josepph Sinde Walioba akizungumzia rasimu hiyo ya katiba alisema kuwa rrasimu hiyo ilikuwa imepunguza sana madaraka ya rais na hivyo itaondoa hofu ya wananchi kuwa rais alikuwa na madaraka makubwa sana.

Kikao hicho kimekamilika leo na rais amewataka viongozi wanaohusika kuitoa rasimu hiyo kwenye mitandao ili kuwafanya wananchi waisome kwa undani zaidi.