HUKU Dk. Damas Ndumbaro, akiwa amekata rufaa kupinga adhabu ya kifungo cha miaka saba kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi iliyotolewa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amesema ataendelea kufanya kazi zake za kuwawakilisha wadau wa soka watakaohitaji huduma yake ya uwakili.
Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Ndumbaro alisema kuwa TFF na Kamati zake hazina mamlaka ya kumfungia kufanya kazi za uwakili, isipokuwa Jaji Mkuu wa Tanzania na serikali.
Dk Ndumbaro akiwaonyesha Waandishi wa Habari hati iliyosainiwa na klabu
Ndumbaro alisema kuwa anashangaa kuona amehukumiwa na Kamati ya Nidhamu kwa kosa la maadili na kuongeza kwamba kamati hiyo haikupaswa kusikiliza tuhuma zilizokuwa zinamkabili.
Alisema kuwa adhabu hiyo aliyopewa ni dalili za wazi za 'chuki' dhidi yake kwa sababu yeye alichokizungumza ilikuwa ni maamuzi ya klabu 12 za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambazo zilikubaliana na kumteua yeye kupitia Kampuni yake ya Uwakili ya Maleta & Ndumbaro ya jijini.
"Sikuzungumza kwa niaba yangu, nilikuwa na ridhaa ya klabu 12, isipokuwa Stand United na Coastal Union, Kamati hii inatumiwa na Jamal Malinzi, ndio kamati iliyoipa ushindi Stand United kupanda Ligi Kuu," alisema Ndumbaro.
Wakili huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba alisema kuwa alianza kuonekana ni adui mara baada ya kukataa kushiriki katika ufujaji wa fedha ambapo kwa vipindi vitatu tofauti alikataa kusaini hundi za fedha ambazo TFF iliomba kutoka kwenye Bodi ya Ligi Kuu (TPL).
Alisema kwamba kwa sasa shirikisho hilo linakabiliwa na ukata baada ya kutumia kiasi cha Dola za Marekani 696,823 bila ya kupata kibali cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao wamezitoa kwa ajili ya udhamini wake wa timu ya Taifa (Taifa Stars).
Mbali na matumizi hayo, pia Jamal Malinzi anadaiwa kujilipa binafsi Dola za Marekani 159,140 ndio maana sasa wanaamua kufidia fedha hizo katika gharama nyingine ikiwamo makato ya Sh.1,000 kwa kila tiketi," alisema Ndumbaro.
Aliongeza kuwa anashangaa kuona TFF inaendelea kukata Sh. 1,000 katika kila tiketi za mashabiki wanaoingia uwanjani kushuhudia mechi za Ligi Kuu Bara na kutaja kiasi kilichokatwa hadi kufikia jana ni Sh. milioni 193.2 zilizotokana na mashabiki 193,257 walioingia viwanjani kushuhudia michezo ya ligi iliyoanza Septemba 20 mwaka huu.
Alisema pia anashangaa kuona rufaa yake aliyokata tangu Oktoba 21 mwaka huu haijapangiwa siku ya kusikilizwa lakini kikao cha Kamati ya Nidhamu kilichokutana kumjadili kilichukua siku mbili.
Aliongeza kuwa leo Oktoba 31 mwaka huu siku ya 10 na hakuna dalili za kusikilizwa, tutaendelea kuhesabu, mambo mengi yako katika rufaa.
Alisema kwamba yeye hajawahi kutoa siri za shirikisho na kueleza kuwa kanuni za ligi na mikataba inayoingiwa si siri.
KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Ijumaa, 31 Oktoba 2014
Alhamisi, 30 Oktoba 2014
DU!!MKE AMUANDALIA MUMEWE MKOROFI CHAKULA CHA KONDOMU
Watu wangu makini mmeisikia hii kutoka BBC ya mama alieamua kummuandalia mume wake mkrofi chakula cha mipira inayotumiwa wakati wa kufanya ngono!isome hapa:
Mwanamke mmoja mwenye watoto watatu katika wilaya ya Kole nchini Uganda alimuandalia mumewe mlo wa mipira ya kondomu kufuatia ugomvi usiokwisha kati yao.
Mwanamke huyo ambaye ni mkaazi wa eneo la Arao aliripotiwa kununua paketi tatu za kondomu aina ya "Trust" kutoka duka jirani kabla ya kuzipika na kumuandalia mumewe kama chakula baada ya kurudi nyumbani akiwa amelewa chakari.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda, mwanamke huyo aliikata kata mipira hiyo ya kondomu ambayo ilikuwa haijatumika katika vipande vidogo vidogo na kuvichemsha kwa muda kabla ya kuvikaanga kwa mafuta ya kupikia na viungo vingine.
Wakati mumewe alipowasili kutoka kubugia pombe katika eneo jirani la kibiashara la Odede,aliandaliwa mlo huo katika sahani tofauti moja ikiwa na mipira hiyo kama mboga na nyingine ikiwa na mkaa.
Lakini jamaa huyo alibaini njama za mkewe baada ya kuonja mlo huo na kugundua ulikuwa na ladha tofauti.
Hatua hiyo ilikuwa ikilenga kumfunza mume huyo ambaye amedaiwa kuzua ugomvi na mkewe kila anapolewa na kurudi nyumbani.
CREDIT; HABARI NA PICHA KUTOKA BBC
HII NI KALI NYINGINE!!KUFANYA MAPENZI NA WANAWAKE WENGI TIBA YA CANCER!!
Kulala na wanawake wengi kunapunguza hatari ya kupatikana na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo,kulingana na utafiti.
Katika utafiti uliochapishwa katika jarida la saratani,Watafiti kutoka chuo kikuu cha Montreal wamebaini kwamba ikilinganishwa na wanaume walio na mpenzi mmoja katika maisha yao yote,kulala na zaidi ya wanawake 20 kunapunguza uwezekano wa kupatikana na ugonjwa huo kwa asilimia 28.
Wanaume 3,208 walishiriki katika utafiti huo ambapo kati yao Wanaume 1,590 walipatikana na ugonjwa huo kati ya Septemba mwaka 2005 na Agosti mwaka 2009.
Kwa jumla watafiti hao walibaini kwamba wanaume wenye saratani ya kibofu cha mkojo kuna uwezekano mara mbili kwa wao kuwa na watu wa familia zao wenye saratani.
Hatahivyo ushahidi unaonyesha kwamba idadi kubwa ya wapenzi wa kike miongoni mwa wanaume inapunguza tishio la ugonjwa huo.
Mwanamume anapojamiana na zaidi ya wanawake 20 katika maisha yake,tisho la kupata ugonjwa huo linapoungua kwa asilimia 28 mbali na asilimia 19 kwa aina yoyote ya ugonjwa wa saratani.
Utafiti huo pia umebaini kwamba mmoja kati ya wanaume wanne wa kiafrika hupatikana na saratani
CREDIT:PICHA NA HABARI KUTOKA BBC.
HII NAYO KALI!!MKURUGENZI WA KAMPUNI YA APPLE INAYOTENGENEZA SIMU ZA IPHONE AJITANGAZA KUWA SHOGA
Mkurugenzi wa kampuni kubwa ya simu duniani ya APPLE inayotengeneza simu za IPHONE bwana TIM COOK leo ameishangaza dunia baada ya kujitangaza hadharani kuwa ni shoga.
Cook amesema kuwa amekuwa akiwaambia wafanyakazi wenzake kuhusiana na hali yake hiyo ya kimahusiano lakini hajawahi kuwa wazi hadharani na sasa ameamua kuuambia ulimwengu kuwa yeye nia shoga.
''Nimekuwa nikiwaambia wafanyakazi wenzangu na wote wanajua hali yangu ya kimahusiano lakini sijawahi kuliweka swala hili hadharani lakini naomba kuitumia nafasi hii kusema kuwa mimi ni shoga na najivunia kuwa hivyo na kumshukuru MUNGU kwa zawadi hii kubwa aliyonipa'',alisema bwana cook!! Ajabu ee!.
Jumanne, 28 Oktoba 2014
KUHUSU FEDHA ZA MUIMBAJI HARRYSONG INSTAGRAM
Muimbaji huyo alisema kuwa kamwe hawezi kufanya ujinga wa kuazima pesa na kupiga nazo picha kwa kuwa kitendo hicho hakitakuwa na maana yoyote kwake.
AUSTRALIA YAPIGA MARUFUKU NDEGE KUTOKA NCHI ZA AFRIKA MAGHARIBI
Akizungumza na vyombo vya habari,waziri anaehusika na maswala ya uhamiaji bwana Scott Morrison amesema kuwa hakutakuwa na visa mpya zitakazotolewa kwa wasafiri wa nchi hizo na zile ambazo ziko kwenye mchakato zitazuiwa.
Nchi ambazo zimepigwa marufuku ni pamoja na sierra leone,guinea pamoja na Liberia.
OZIL AONESHA PICHA ANAVYOENDELEA VIZURI NA MATIBABU
Hayo yamethibitika baada ya kuandika maneno haya katika ukurasa wake wa face book;
''best team! Thanks for your great support to enable my quick recovery''
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)






