Kurasa

Ijumaa, 23 Machi 2018

MWALIMU KUTEGEMEA VIBOKO NI KUKIRI UDHAIFU.

 

 Walimu pamoja na wazazi Tanzania tumekuwa na utaratibu ambao sasa umegeuka kuwa utamaduni wetu wa kutumia viboka kuwaadabisha watoto wetu. Wakati huohuo sisi watu wazima tulikataa utaratibu huo kwa nguvu kweli wakati wakoloni walipokuwa wanautekeleza kwetu.( hii inachekesha kweli).Mala nyingi nimekuwa nikiwaambia watoto wadogo kuwa sio vizuri kumfanyia binadamu mwenzako kile ambacho usingependa wewe kufanyiwa. Kwanini sisi tunawafanyia watoto wadogo matendo haya!!.

Kila binadamu kulingana na umri alionao ikiwa ni mtoto,kijana au mzee ana mapungufu ambayo binadamu wa umri mwingine hawayapendi.Vijana wanafanya mambo ambayo wazee hawapendi,Wazee hufanya mambo ambayo watoto hawapendi na ndio mana wakati mwingine utamsikia mtoto anauliza swali kama, kwa nini mzee yule anakunywa pombe au anampiga mama yake Bakari kila siku??. Sasa je watoto nao wakiona wazee au vijana wanafanya makosa kwa nini wasiruhusiwe kuwachapa wazee?? au ndio ile sheria ya mwenye nguvu ndio atasurvive.

KWA WALIMU; Hebu jaribu kujipima uwezo wako wa kumsaidia mtoto kuwa na tabia njema bila kumuumiza.Mimi nilikuwa moja kati ya walimu wanao amini sana viboka.Sasa hivi nikimuona mwalimu anamchapa mwanafunzi namuona kama mwalimu aliefell kila kitu na hata hastahiri kumfundisha mwanafunzi jinsi ya kuendesha maisha na kuwa mtu mwenye furaha wakati yeye anashindwa kumfurahisha mwanafunzi huyo. Ukiweza hasa kuzifuata mbinu mbali mbali za kuwasaidia wanafunzi kuwa na tabia njema utajikuta unaipenda kazi yako kiasi kwamba hata ukiwa ni siku ya kufunga shule unjisikia kulia kwasababu wanafunzi unawaona kama familia yako na wanajisikia hivyo hivyo. Hakuna kitu ninachofurahi kila siku asubuhi nikienda kazini kama kuona kundi la wanafunzi wakinishangilia baada ya kuniona mwalimu wao nawasili kazini. TUACHE KUWAFANYA WANAFUNZI MAADUI ZETU KWASABABU HUWEZI KUMFUNDISHA ADUI YAKO AKAKUELEWA. Sitaki kuwaacha walimu hapa bila kuwapa kamfano ka jinsi unavyoweza kusaidia tabia njema kwa wanafunzi; Soma tabia za wanafunzi wako wote na ujue kila mmoja anapenda nini.Mwanafunzi anapokosea jambo mwambie siku hiyo hatafanya kile anachokipenda ikiwa ni kucheza mpira au rede. Huu ni mfano tu wa adhabu ambazo hazimuumizi mwanafunzi mwili wake bali zinampa motisha kufanya vizuri.Zipo nyingi ambazo kama mtu anahitaji msaada anaweza kunitumia ujumbe kwenye 0626641484 tukakubaliana jinsi ya kusaidiana kwa hili. MOJA KATI YA MAMBO NINAYO YAPIGANIA SASA HIVI NI KUPATA MSAADA KUTOKA KWA WADAU WA ELIMU TUWEZE KUWA NA MADARASA AMBAYO YATAKUWA KAMA YA MFANO WA JINSI YA KUWAFUNDISHA WATOTO WAKIWA NA FURAHA,HURU NA KUIJUA THAMNANI YA ELIMU.Kama wewe ni mmoja wapo pia tafadhari usisite hakuna juhudi inayopotea bure.

KWA WAZAZI; Tafadhari sana wazazi msitumie watoto kama sehemu ya kumalizia hasira zenu.Watoto wanarugha mbalimbali ambazo zinaashiria upendo na kila mmoja anarugha yake ambayo ukiigundua ukaifanyia kazi basi mtoto huyo atafanya unachotaka badala ya kumpiga mifimbo kila siku.
Mfano kuna watoto (pamoja na watu wazima) ambao lugha yao ya upendo ni Zawadi.Yani mtoto huyu au mtu huyu ukiwa unampa zawadi basi mwambie chochote atakuwa anakufanyia kwasababu unampa furaha ya maisha yake.LUGHA HIZI ZA UPENDO ZIKO TANO NA KILA BINADAMU ANA LUGHA YAKE. Wazazi pia kama unataka kujua zaidi kuhusu lugha za upenda kwa mwanao na mkeo au mumea na jinsi ya kuzitumia ukapata faraja ya maisha na mtoto akaacha kukusumbua nitumie ujumbe ili tujue tunasaidiana vipi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni