Kurasa

Jumamosi, 9 Aprili 2016

UTAJIRI #WEALTH#

PICHA;WARREN BUFFETT.MMOJA WA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI.

Karibu sana mpenzi msomaji katika muendelezo wa mada zetu ambazo zinahusu Biashara na ujasiriamali,mada ambazo zinapatikana katika kitabu chetu kinachouzwa kwenye mtandao kinachoitwa MIMI NI TAJIRI.Tunashauri wasomaji wetu kuanza kusoma mwanzo kabisa wa mada hizi ambazo tulianza kwa kuangalia maana ya ujasiriamali,jinsi ya kupata mitaji na makao ya biashara.Pamoja na hayo pia kuna mafunzo ya jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo Batiki na Sabuni za aina mbalimbali.

Leo tunaendelea na mada yetu tuliyoianza inayohusu UKWELI KUHUSU UTAJIRI. ambayo tuliishia kwa kuona ni jinsi gani unaweza ku adopt mazingira yakakufanya kuwa Tajiri.


Ukitaka kujua siri iliyopo kuhusu ukweli huo fikiria kuhusu mwili wa binadamu.Wakati kunapokuwa na baridi kali vinyweleo vya ngozi husimama kukinga joto lililopo ndani ya mwili lisitoke nje lakini pia baridi iliyoko nje isipenye ndani ya mwili.Wakati wa joto mwili hutoa  jasho ambalo hufanya kazi ya kuupoza mwili na linapokauka mwili huwa baridi kabisa.Kama hiyo haitoshi unapobeba vitu vizito mwili hujitengenezea nguvu ya ziada na misuri kutanuka ili uweze kuhimili uzito wa mizigo hiyo.
Hivi ndivyo pia akili ya binadamu ilivyo.Inaweza kubadilika kulingana namazingira yaliyopo,na ikifundishwa kitu chochote kile hukichukua na kukiishi.

THAMANI YA CHANGAMOTO;
Moja kati ya matajiri wakubwa duniani aliwahi kuulizwa kitu anachokipenda zaidi katika maisha yake na akajibu kuwa anapenda sana changamoto.Mimi namuongezea tajiri huyo kwa kusema kuwa maskini mwenye changamoto nyingi anaweza kuwa tajiri mkubwa kuliko tajiri mwenyewe.
Tunapaswa  kujiuliza maswali kwamba ingekuwa vipi kama duniani kusingekuwa na changamoto? Sidhani kama dunia ingekuwa inapendeza hivi ilivyo.Wala ugunduzi wa vitu vya ajabu kama umeme,compyuta,simu,nyumba kubwa na nzuri,magari nk ungekuwepo.
Historia inaonesha uwa watu na mataifa yaliyokumbwa na changamoto nyingi hapo zamani zikiwemo changamoto za kimazingira na Rasilimali,ndio watu au mataifa yaliyoibukia kuwa matajiri sana.Mfano wa mataifa hayo ni mataifa ya Magharibi kama Uingereza na Marekani.
Akili ya binadamu ina kazi moja kubwa ambayo ni kupata changamoto na kuzitafutia ufumbuzi.Zinaweza kuwa changamoto ndani ya mwili au nje ya mwili.Kwa jinsi changamoto inavyokuwa kubwa ndivyo akili inavyotumia nguvu nyingi kupata ufumbuzi.Bahati nzuri ni kuwa changamoto zinavyokuwa kubwa ndivyo akili ya binadamu inavyokomaa na kuwa na uwezo zaidi.
Hii maana yake ni kuwa badala ya kumlaumu Mungu kwa kuziweka changamoto tunapaswa kumshukuru kwasababu ni kama ametuwekea daraja la kuvuka kutoka ng'ambo moja ya mto kuelekea ng'ambo nyingine.
Tunapaswa kufikiria nje ya box ambapo badala ya kufikiria kuna mambo mabaya katika maisha yetu tunapaswa kuyageuza kuwa baraka na hakika zitakuwa baraka..Kumbuka kila kazi ya binadamu inayoonekana katika uso wa ardhi ilianza na wazo la mtu mmoja katika kichwa chake.Akili yako bado haijatumika kabisa na una deni kubwa sana katika maisha yako.
Ifikirie akili iliyotengeneza umeme,Simu,computer,magari,ndege nk,halafu ifikirie akili yako imetengeneza nini walau cha kusifiwa na jamii unayoishi achilia mbali dunia.Bado hujachelewa,anza sasa safari ya kufanya kitu ili na wewe ufeukiwa umeitendea haki dhamira ya MUNGU kukuumba na akili nzuri.
Mpenzi msomaji kwa leo tumefika mwisho tukutane wakati mwingine kwa muendelezo wa mada hizi za biashara na ujasiriamali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni