visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumanne, 12 Aprili 2016

NENO SMART NA MAANA YAKE KATIKA BIASHARA. #THE WORD SMART AND ITS MEANING IN BUSINESS#



.

Watu wengi tumekuwa tukilitumia neno SMART kuonesha jinsi mtu alivyo msafi na nadhifu.Lakini katika mafanikio wataalamu wanasema katika neno SMART kuna herufi tano(5) ambazo kama mtu atazifuatilia kwa makini atakuwa ni mtu mwenye mafanikio yasiyo kifani.Katika neno hili kuna herufi za kiingereza ambazo kila herufi inawakilisha neno muhimu sna katika maisha.Maneno hayo ni SPECIFIKI AU MSIMAMO,MEASURABLE AU INAYOPIMIKA,ATTAINABLE AU INAYOFIKIKA,REARISTIC AU HALISIA NA TIME BOND AU INAYOENDA NA MUDA.Sasa tuliangalie neno mojamoja;


MISIMAMO.
Mala nyingi watu wenye misimamo katika mambo yao hupata mafanikio sana,hususani katika shughuli zao za kujipatia kipato.Unapaswa kufanya jambo moja kwa wakati mmoja badala ya kufanya mambo mengi ambayo kutokana na wingi wake unakosa umakini na kuyafanya ovyoovyo.Kwa mfano jaribu sana kuepuka swala la kubadilisha badilisha biashara na badala yake biashara yako inapopitia changamoto jaribu kuzitatua changamoto hizo kwani kwa jinsi unavyotatua changamoto mbalimbali ndivyo unavyozidi kujielimisha na kupata ujuzi mbalimbali kuhusiana na biashara yako na hatimae utaifanya kwa ufanisi sana.

YENYE KUPIMIKA.
Ni vizuri sana kujiwekea viwango kwa jambo unalolifanya na kujipima kila baada ya mda fulani.Kama mfanyabiashara unapaswa kulenga biashara yako kufikia viwango fulani vya ubora ambavyo mala nyingi huwa ni dira ya biashara yako.Hii haina tofauti sana na malengo ya muda mfupi na mrefu ya biashara yako            ambayo utayatumia kupima muelekeo wa biashara yako kama unakwenda mbele au inarudi nyuma

UHALISIA.
Kama mfanyabiashara unapaswa kuwa halisi na mkweli kwako mwenyewe na kwa biashara yako.Maana yake ni kuwa kama biashara yako ina changamoto ukubali kuwa changamoto zipo na uwe tayari kuzitafutia ufumbuzi.Pia usilazimishe kuwa na matumizi makubwa ya pesa wakati faida unayopata ni ndogo.Jambo hilo linaweza ukuleta matatizo kwako na kwa biashara yako.Epuka kutaka mambo makubwa ambayo kiukweli huna uwezo nayo kwasababu yanaweza kukurudisha nyuma kibiashara.

MUDA.
Imekuwa ni utamaduni kwa wazungu kuwa na saa katika mikono yao hata kama wanakuwa na simu za mikononi.Hii inadhihirisha umuhimu wa muda kwa watu hawa ambao wametuacha mbali katika mafanikio.
Hii ni moja kati ya nguzo muhimu sana kwa mjasiriamali au mfanyabiashara.Kila jambo unalofanya kama mfanyabiashara unapaswa kulipangia muda wake kulitimiza.Hii itakusaidia kuyaweka katika vitendo malengo yako na mipango yako.Kwa bahati mbaya ni kuwa sisi waafrika tumekuwa na tabia ya kufanya mambo bila kujali muda.Ndio maana ni rahisi sana kwa Mwafrika kuahirisha jambo lililopangwa endapo kuna jambo litatokea katikati.

Bahati nzuri ni kuwa hata kama unatabia ya ukutokujali muda bado una uwezo wa kubadilika na kuwa mmoja wa watu wanaojali sana muda na hatimae kuwa na mafanikio.

Kwa vipi...............

Wataalamu wanasema kuwa bianadamu akifanya jambo ndani ya siku 21,inageuka kuwa tabia.Jaribu kuamka kila siku saa kumi na nusu na kufanya mazoezi.Baada ya hapo jaribu kuweka kila kitu katika mpangilio wa muda utaona matokeo yake.

Kwa kawaida mtu anaeweka mambo yake katika muda huwa ni rahisi sana kuyatekeleza na sio rahisi kwa mtu huyo kuchezea muda bila kufanya mambo ya msingi.Kuna watu wamekuwa mahiri sana kulaumu watu wanaoshabikia mipira na wakati huohuo yeye pengine ni mlevi na anatumia masaa mengi na pesa nyingi sana katika ulevi!!. Tatizo kubwa hapa sio pombe wala ushabiki,tatizo ni mpangilio wa nyakati.Hii ndio sababu kuna mashabiki wa mipira ambao ni matajiri sana akiwemo msanii JAY Z ambae ni mshabiki mkubwa wa timu ya ARSENAL,Lakini pia kuna matajiri wengi sana ulimwenguni ambao ni walevi kupita kiasi.
PICHA; MSANII JAY Z MOJA KATI YA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI.

Ni vizuri sana kuwa wa kwanza katika kila jambo unalokusudia kufanya au ambalo lipo kwenye ratiba zako za siku.Hii itakuongezea imani kwa watu,kukupa morali na kukuongezea ufanisi.

Mpendwa msomaji kwa leo tunaweka kituo kikubwa hapa.Kwa wale wageni jitahidi kusoma mada hizi zote kuanzia mwanzo mpaka hapa tulipofikia.Angalia upande wa kulia wa blog hii utakutana na machapisho yaliyopita ya mwaka 2016 utakutana na mada zote zinazohusu ujasiriamali na biashara,soma zote ili upate mfululizo unaostahiri.Kama kuna lolote tutumie ujumbe kwenye 0654627227. usisahau kusoma BLOG HII YA UJASIRIAMALI NA BIASHARA MALA KWA MALA INAYOONGOZA KWA SASA TANZANIA 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni