Kurasa

Jumanne, 19 Aprili 2016

MISINGI YA MAFANIKIO. #THE FOUNDATION TO SUCCESS#

3d white business person in a job interview with the curriculum vitae and social networks profile  3d image  Isolated white background   Stock Photo - 16723453
PICHA(www.123rf.co);INTERVIEW KIKIWA NI KIPIMO KIMOJAWAPO CHA KUMPA MTU KAZI.

Hujambo mpendwa msomaji na karibu tena katika mfululizo wa mada zetu ambazo kwa wewe unaetembelea mtandao kwa lengo la kuongeza kitu katika maisha yako iwe maarifa au mafanikio utakuwa unafaidika sana na mada hizi ukilinganisha na walio wengi ambao huingia mtandaoni na kutazama mambo ambayo hayana msaada katika maisha yao kimwili,kiakili na kiroho.

Kwa wale wanaofuatilia mada hizi zimekuwa zikiletwa mfululizo kuanzia ujasiriamali ninini? mpaka pale ambapo tutaona mwisho wake ni upi.Kumbuka mada hizi zinapatikana katika kitabu kinachoitwa MIMI NI TAJIRI kinachouzwa mtandaoni.Tunakaribisha yoyote ambae atakuwa tayari kukitoa kitabu hiki katika mfumo wa hard copy awasiliane na sisi.

Leo kama kilivyotangulia kichwa cha Habari tutaangalia Misingi au kanuni za mafanikio katika biashara na mambo mengine.

Kanuni za mafanikio yoyote yale ziko katika maeneo matatu KUJIAMINI,JUHUDI NA UWEZO (KKK).CONFIDENCE,COMMITMENT AND COMPETENCE (CCC).Unaweza kuita kwa jina lingine 3K au 3K.


1.KUJIAMINI..
Hili limeshaongelewa sana katika kitabu hiki.Kwa kifupi kujiamini ni hali ya kuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi magumu sehemu ambayo nafsi yako inakataa.Haina tofauti sana na ujasiri.Mfano watu wengi wamekuwa wakiogopa mikopo mikubwa kwa hofu ya kushindwa kulipa.Anaejiamini badala ya kufikilia kushindwa kulipa huweka mikakati ya kuwa na uwezo wa kulipa hata kama deni litakuwa ni kubwa kiasi gani.
Tunapaswa kujiamini kwa kila tunachokifanya na nakuhakikishia utakuwa ni nyumba ya mafanikio.

2.JUHUDI KATIKA KAZI.
Kazi au biashara yoyote hata iwe ya faida kiasi gani,isipofanywa kwa juhudi na maarifa haiwezi kumfikisha mhusika kwenye malengo anayokusudia.Mfanyabiashara anapaswa kuweka mawazo na akili yake yote kwenye biashara hiyo.Kwa kufanya hivyo ubunifu wa kila aina utawekwa katika biashara hiyo na hatimae kutoa matunda yanayokusudiwa.

3.UWEZO(COMPETENCE)
Fanya kazi au biashara ambayo unahisi ndani ya nafsi yako kuwa unaiweza.Uwezo hufanya usahihi wa kufanya jambo kuwa mwingi katika kazi kuliko mapungufu.
Siku zote epuka kufanya kazi kwa kuiga watu wengine kwa sababu tumetofautiana uwezo wa kufanya mambo mbalimbali na anachokiweza yule wewe unaweza kukishindwa.Jitahidi sana uwezo ulionaokatika kazi unayoifanya unauongeza kwa kujisomea vitabu mbalimbali na kuuliza watu mbalimbali wenye uzoefu katika secta unayofanyia kazi na baada ya muda na wewe utajikuta umekuwa mtaalamu kupita kiasi.

>PENDA UNACHOKIFANYA<
Wataalamu husema mtu yoyote anaefanya kazi anayoipenda ni kama hafanyi kazi.Msemo huu maana yaka ni kuwa mala nyingi mtu anaefanya kazi anayoipenda hujikuta anafanya kazi hiyo muda mrefu huku akijitolea kimwili na kiakili kwasababu ni kama inakuwa hobi na hufurahia kufanya kazi hiyo.Unapofanya kazi usioipenda unaweza usimalize hata saa moja unakuwa umechoka.Hili hutokea kutokana na mwili kujicondition.Chukulia mfano wa mwanamuziki,Ni vigumu sana kwa msanii wa muziki kuchoka anapofanya kazi yake kwasababu asilimia kubwa ya wasanii hao hupenda sana kazi yao hiyo,labda kwasababu kazi yenyewe ni burudani.

Habari nzuri ni kuwa unaweza pia kuipenda kazi ambayo pengine mwanzoni ulikuwa huipendi.Unapofanya kazi fulani kwa muda mrefu inakuwa sehemu ya maisha yako na hivyo mwili na akili yako hujitengenezea mazingira ya kuikaribisha kazi hiyo na kujikuta unaipenda kuliko awali.

Watu wengi wameshawahi kuanza kuishi na wanawake wasiowapenda lakini baada ya kuishi muda mrefu na kuwazoea hujikuta wanatengeneza upendo na hatimae kuishi raha mustarehe.

Maana ya mfano huo ni kuwa unaweza pia kuanzisha biashara usioipenda lakini ukijifunza kuipenda utaipenda na hutaona kama ni kazi ngumu sana.

JAMII INAYOKUZUNGUUKA NA UMUHIMU WAKE.
Kila binadamu anazunguukwa na jamii ambayo kwa namna moja au nyingine inakuwa inamhusu.Kuna makundi mbalimbali kwenye jamii mengine yakiwa na umuhimu sana kwako na mengine yakiwa na umuhimu wa wastani.Baadhi ya makundi hayo ni kama ifuatavyo;
i)Familia yako
ii)Wafanyabiashara wenzako.
iii)Taasisi za dini
iv)Viongozi wa serikali
v)Watu wenye mahitaji mbalimmbali.

Hya ni baadhi tu ya makundi na yanaweza kuwa na faida na hasara kwenye biashara yako kama ifuatavyo;

  • FAMILIA YAKO
Hili ni kundi muhimu sana kwako na kwa biashara yako.Kama mambo yatakuwa yamekwenda vibaya  ni vigumu sana kufanya vizuri ofisini au hata katika biashara yako.

Jamaa mmoja alifuata kanuni zote za ujasiriamali na hatimae akawa tajiri kupita kiasi.Kwa bahati mbaya kutokana na maisha aliyokuwa akiishi na mkewe alijikuta anapoteza utajiri wote kwa mkewe.Mwanamke huyo alikuwa anakorofishana mala kwa mala na mkewe na kutokana na hilo alipanga kudai taraka.Aliajiri wakili kwa kutumia fedha za mumewe na kufungua kesi mahakamani ya kudai taraka na kuomba fidia.Mwanamke huyo alishinda kesi na hatimae jamaa yule alifilisiwa utajiri wake na mahakama na akapewa mkewe.

Kilichokuwa kinatokea katika mfano huu ni kuwa yule jamaa alitelekeza familia yake akapeleka mawazo yake yote katika biashara.Kutokana na hilo alifanikiwa kibiashara lakini alishindwa kijamii.
Unapaswa kuipa umuhimu wa juu sana familia yako kama unavyozipa umuhimu biashara zako.Kwa kifupi ili biashara zetu zifanikiwe ni lazima kwa kiasi kikubwa kushirikisha familia zetu.

  • WAFANYABIASHARA WENZAKO.
Hawa ni watu muhimu pia kwako.Unahitaji kujifunza mengi kutoka kwao.Pia wao wanahitaji kujifunza kitu kutoka kwako.Kama mfanyabiashara hupaswi kuwa na uhusiano wa upande mmoja kwa kila kundi katika jamii.Hakikisha na wewe unakuwa na mchango mkubwa katika makundi hayo na hivyo ndivyo jinsi unavyoweza kuimarisha uhusiano wako na makundi hayo la sivyo unaweza kuishia kutengwa kama watagundua kuwa hawanufaiki chochote kutoka kwako.

  • TAASISI ZA DINI.
Kama mfanyabiashara mzuri unapaswa kuwa na imani.Hii ni kwasababu biashara yenyewe ni imani na inahitaji mtu anaeamini.Mfano,mfanyabiashara wa duka anapotoka nyumbani kwake asubuhi kwenda dukani hajui ni wateja gani au wangapi watakuja dukani kwake lakini bado anakwenda dukani akiamini kuwa lazima wateja watakuja.

Ni vizuri sana kushiriki ibada na shughuli nyingine katika dini unayoiamini na hii hatimae itakusaidia kuimarisha imani yako kiroho.Faida za imani ni kukutengenezea uvumilivu na matumaini katika biashara na hivyo itakuondolea roho za kukata tamaa na utasonga mbele hata kama mambo yatakuwa magumu kiasi gani.

  • VIONGOZI WA SERIKALI.
Huwezi kuwakwepa hawa katika biashara.Lazima utakutana nao katika kulipa kodi au mambo ya afya za jamii au leseni pamoja na vibari mbalimbali vya kibiashara.

Hakikisha unakuwa na mahusiano pamoja na mawasiliano mazuri na viongozi au maafisa wa serikali.Hii itaifanya biashara yako kuwa salama na wewe kuifanya kwa uhuru zaidi.

  • WATU WENYE MAHITAJI.
Katika biashara yoko utakutana na watu mbali mbali wakikuomba uwasaidie kutatua mahitaji yao japo kidogo.Utapaswa kuwa mtoaji pia.Sio kutoa kila kitu bali kujitahidi kutoa michango kwa wahitaji mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine watahitaji msaada wako.

KUMBUKA;
Unapaswa kuhakikisha kuwa unaempa msaada,kweli anastahili kusaidiwa na sio tapeli.

Asante sana mpendwa msomaji kwa kutufuatilia kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mada hii.Wakati mwingine tutaangalia mada ya afya zetu na umuhimu wake katika biashara zetu.Kama kuna lolote unaweza kuwasiliana nasi kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba0654627227.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni