Kurasa

Jumamosi, 18 Oktoba 2014

WASICHANA WALIOTEKWA NA BOKO HARAMU KUACHIWA HURU

Serikali ya Nigeria na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram, wamefikia makubaliano ya usitishaji mapigano na kuachiliwa huru wanafunzi wa kike wanaoshikiliwa na kundi hilo.
Hayo yameelezwa na mkuu wa vikosi vya jeshi la Nigeria, Meja Jenerali Alex Sabundu Badeh na Hassan Tukur, Katibu wa ikulu ya rais ya nchi hiyo na mshauri wa karibu Rais Goodluck Jonathan na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa makubaliano hayo, kundi hilo litatakiwa kuwaachilia huru wasichana hao zaidi ya 200 liliowateka nyara tarehe 14 Februari mwaka huu huko Borno.
Inaelezwa kuwa pande hizo mbili zimefikia makubaliano hayo Ijumaa ya jana, baada ya mazungumzo yaliyofanyika nchini Saudi Arabia ambayo yalijumuisha Rais wa Chad, Idris Deby na maafisa wa ngazi ya juu kutoka Cameroon.
Wakati huo huo jeshi la Cameroon limetangaza kuua wanamgambo 107 wa Boko Haram, katika mapigano yaliyojiri kati ya pande mbili huko kaskazini mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo, mapigano hayo yalitokea asubuhi ya siku ya Jumatano miji ya Amchide na Limani iliyoko mpakani kati ya nchi hiyo na Nigeria.
Wizara hiyo imeongeza kuwa, katika mapigano hayo yaliyoibuka baada ya wanamgambo wa Boko Haram kuvuka mpaka na kuingia nchini Cameroon, yalipelekea kuuawa askari wanane na raia saba wa nchi hiyo.
BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni