Kurasa

Ijumaa, 10 Oktoba 2014

BASI ALILOPANDA BABA LEVO LAPATA AJARI AKIELEKEA MPANDA

BreakingNews, stori kubwa
Baba LevoNi saa tisa kasoro mchana Msanii wa bongofleva Baba Levo anapiga simu na kuongea kwa tabu kwenye usikivu ulio mdogo na kusema kwamba amepata ajali kwenye pori karibu na eneo linaitwa Uluwila akiwa anatokea Tabora kwenda Mpanda.
Alikua kwenye Basi liitwaloAMambapo ghafla wakiwa kwenye kona ilitokea Coaster ikiwa na abiria ambayo dereva wake alikua akikwepa barabara mbovu hivyo ikabidi ahamie kwenye upande wa pili wa barabara ambako ndiko lilikua linapita basi la kina Baba Levo ambalo hakuliona sababu ni kwenye kona.
Dereva wa basi la kina Baba Levo ilibidi ahame upande wake ili ahamie kwenye upande wa magari yanayopanda ambao ndio upande sahihi wa ile Coaster kupita ambapo juhudi zake hazikufanikiwa kwani wote walikua kwenye spidi na yule dereva wa Coaster alihama kwenye ule upande baada ya kuona atagongana uso kwa uso na basi la kina Baba Levo ila bahati mbaya wakawa wote wamejikuta upande mmoja na wakagongana uso kwa uso.
Mwenye makosa anatajwa kuwa ni mwenye Coaster ambapo pamoja na Baba Levo kuumia usoni na mwilini kwa kuchanwachanwa na vioo vya mbele vilivyopasuka kwenye basi, ameweza kuona kuna baadhi ya watu wamefariki ambapo kati yao ni waliopasuka vichwa na shingo.
Dereva wa basi la kina Baba Levo hajaumia sana wala basi halijaumia sana, Coaster ndio imefumuka upande wa juu wote na kuharibika sehemu nyingine pia huku kilichosababisha Baba Levo kuumia ni kwamba alikua amekaa pale juu ya Injini ya Basi kwenye kigodoro kutokana na basi hilo kujaa.
Baba levo anajisikia vibaya kiasi na kwa sasa yuko na wenzake kama 20 pamoja na Askari mwenye silaha waliekua pamoja kwenye Basi…. wanatembea kutafuta kijiji chenye network ili kuomba msaada manake baadhi ya abiria wamebanwa kwenye hiyo Coaster na hawajatolewa.
Credit:millardayo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni