Kurasa

Jumatano, 8 Oktoba 2014

BABA AMCHINJA MWANAE NA KUMTOBOA TUMBO SENGEREMA

Baba mzazi mkazi wa Sengerema anadaiwa kumuua mwanaye wa miaka minne kwa kumchinja koromeo na kumchoma kwa kisu kwenye kitovu na utumbo kutoka nje.
Mzazi huyo anadaiwa kufanya mauaji hayo juzi alfajiri baada ya kumchinja aliuchoma kwa kisu mwili wa mtoto huyo sehemu mbalimbali ikiwemo masikioni na kifuani.
Gazeti la MWANANCHI ambalo lilikua shuhuda limedai baada ya kufanya kitendo hicho alianza kufukuza wananchi waliokusanyika eneo hilo kwa kuwatishia kuwachoma na kisu.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo alizidiwa nguvu na wananchi na kuanza kumshambuliwa kwa kipigo hadi alipookolewa na Mwenyekiti wa mtaa.
Mama mzazi wa watoto hao alisema kabla ya kutengana na mumewe huyo alizaa nae watoto watatu na kwamba ameshangazwa kupata taarifa za mwanaye kuuawa na baba yake.
Jeshi la Polisi linamshikilia kwa uchunguzi huku likisubiri taarifa ya hospitali kuhusu utimamu wa akili yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni