Kurasa

Jumanne, 28 Oktoba 2014

AUSTRALIA YAPIGA MARUFUKU NDEGE KUTOKA NCHI ZA AFRIKA MAGHARIBI


Nchi ya Ausralia imepiga marufuku ndege zote kutoka Afrika magharibi kuingia nchini humo katika harakati za kupambana na ugonjwa hatari wa Ebola.

Akizungumza na vyombo vya habari,waziri anaehusika na maswala ya uhamiaji bwana Scott Morrison amesema kuwa hakutakuwa na visa mpya zitakazotolewa kwa wasafiri wa nchi hizo na zile ambazo ziko kwenye mchakato zitazuiwa.

Nchi ambazo zimepigwa marufuku ni pamoja na sierra leone,guinea pamoja na Liberia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni