Kurasa

Jumapili, 5 Oktoba 2014

AJIUA KWA MOTO KISA WIVU WA MAPENZI

MKAZI mmoja wa kijiji cha Malolwa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Ndikile Sunguli (38) amejichoma ndani ya nyumba hadi kufa baada ya kumjeruhi mke wake katika ugomvi unaoaminika ni wa mapenzi.
Tukio hilo la kutisha lilitokea Septemba 29, 2014 majira ya saa tano usiku katika kijiji cha Mlolwa.
Imeelezwa kuwa Sunguli alirudi kutoka matembezini akiwa amelewa huku akipiga makelele, alipofika nyumbani kwake alianza malumbano na mke wake huku kila mmoja akimtuhumu mwenzake kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Jacob Mwaluanda alisema kuwa wakati ugomvi ukiendelea Sunguli alichukua kisu na kumchoma mkewe wake ubavuni na kumjeruhi.
Kamanda alisema kuwa katika harakati za kujiokoa mama huyo alianguka nje ya nyumba yao na kuzirai, hali inayodhaniwa ilisababisha mume kudhani ameua na kujifungia ndani na kuwasha moto akiwa ndani.
Alisema kutokana na nyumba hiyo kuezekwa kwa nyasi ilishika moto kwa kasi na juhudi za majirani kumuokoa ziligonga mwamba kutokana na kujifungia.
Kamanda Mwaluvanda alisema hali ya majeruhi inaendelea vizuri kwani alikimbizwa kituo cha afya Mpui baada ya tukio hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni