Kurasa

Jumanne, 23 Septemba 2014

KIJANA AMKODISHA MCHUMBA WAKE APATE PESA YA KUNUNULIA SIMU

Mwanafunzi wa Chuo kikuu kimoja cha China ambaye jina lake halikutambulika kwa haraka ameamua kufanya ‘uchizi’ ili mradi tu aipate pesa ya kununua aina mpya ya iPhone iliyoingia sokoni, iPhone6.
Kijana huyo wa alionekana akiwa nje ya chuo kikuu cha Songijiang akiwa na bango kubwa lililoandikwa kwa kichina na kutafsiriwa ‘Girlfriend Sharing’.
Katika tangazo hilo kijana huyo anaeleza kuwa yuko tayari kumkodisha mpenzi wake kwa mtu yeyote atakayeweza kutoa pesa ili jamaa apate kiasi cha kutosha kuinunua iPhone 6 yenye screen kubwa.
Picha ya kijana huyo imesambaa kwa kasi katika mtandao wa kijamii unaotumiwa na wachina uitwao ‘Weibo’ ambao ni kama Twitter.
Tangazo hilo limeambatana na picha za mpenzi wake na amewatoa hofu wateja wanaosita kuingia nae mkataba kuwa hata mpenzi wake ameridhia na yuko tayari kudate na mtu yeyote atakaejitokeza.
Muda wa kuwa na msichana huyo baada ya kumkodi umebainishwa kutokana na malipo yatakayofanywa na mteja. Viwango ni vya saa 1 (10 yuan), siku 1 (50 yuan) au mwezi mmoja (500 yuan).
Hata hivyo, wapenzi hawa sio wa kwanza kujiweka sokoni ili wapate bidhaa ya kampuni ya Apple. Mwaka jana katika uzinduzi wa iPhone 5, wanandoa wa Shaghai waliwaweka sokoni watoto wao watatu ili wapate pesa ya kununua computer na simu za iphones lakini walikamatwa na kufunguliwa mashitaka.
Lakini pia kijana mdogo wa Hunan alijitolea kuuza figo lake ili apate pesa ya kununua iPad na iPhone.
Siyo hayo tu, hivi karibuni mwanaume mmoja wa Saudi Arabia ametaka kupewa iPhone 6 kama mahari ya dada yake hata kabla aina hiyo ya simu haijazinduliwa Bahrain.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni