Kurasa

Jumapili, 7 Septemba 2014

KIGWANGALLA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS

September 7 2014 Dr. Hamisi ambae ni mbunge wa Nzega kwa ruhusa ya CCM alikutana na Waandishi Dar es salaam akiwa ameongozana na mke wake pamoja na watoto wao na kisha kuweka wazi kwamba yuko tayari kugombea kiti cha Urais kwa tiketi yaCCM 2015.
Yafuatayo ndio ameyasema:
1.‘Leo nitasema neno zito kidogo, litabadilisha sura ya historia yangu milele… kinachotokea hapa kina maana kubwa sana kwa watu wenye historia inayofanana na mimi, wale ambao wameyajua maisha ya shida na kukosa uhakika toka wakiwa tumboni mwa wazazi kutokana na hali za uchumi wa familia zao’
2.
‘Nimeyajua maisha ya mtu mnyonge na masikini kwa kuyaishi na sio kwa kusoma ama kusikia, ninajua mtu akiongelea njaa anamaanisha nini’
3.’Watanzania wanataka kupata huduma bora za afya, elimu, maji, miundombinu…… ukienda kwa Wafanyabiashara wakubwa pale Pugu viwandani ama kwa Matabibu wenzangu hospitali ya taifa Muhimbili au kwa Wafanyabiashara pale sokoni Kariakoo wote watakwambia hawapendi kuona kodi zao zikitafunwa na wachache wasio waadilifu’
HK 16
4.’Watu hawatarajii serikali itabeba mizigo yao yote lakini wanaamini kabisa kwamba tukibadili vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha serikali na uchumi wetu, tunaweza kwa kiasi kikubwa kubadili mwelekeo mzima wa maisha ya baadae na kuiondoa Tanzania miongoni mwa nchi masikini kabisa duniani’
1.‘Na mimi kama Watanzania wenzangu wengi nina imani kubwa kabisa kwamba tunaweza kubadili mustakabali wa taifa letu, kufungua milango ya maisha bora zaidi kwa Watanzania, tutatoa fursa sawa kwa kila Mtanzania kuishi kwa matumaini kwamba atabadili maisha yake wakati wowote ule kuanzia leo, tutaweza kuamsha ari ya kila Mtanzania kuongeza bidii kwenye kazi’
‘Ninaamini kabisa kutokea ndani ya mifupa yangu kuwa tukifanya uchaguzi sahihi wa vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha uchumi wetu na serikali yetu……. haya ninayoyasema sio ndoto za mchana’
h13Baada ya kuyazungumza yake ya moyoni baadhi ya Waandishi walipata nafasi ya kumuuliza maswali ambapo hili lilikua mojawapo >>> ‘Umetangaza nia kwamba unagombea Urais lakini sijasikia unapitia chama gani au utasimama binafsi?……… na kama ni chama, mpaka sasa hakuna chama chochote ambacho kimefungua milango kwa Wanachama wake kutangaza nia, kwa kufanya hivyo huwezi kuona unakiuka taratibu za chama?
JIBU:‘Nitapitia chama cha mapinduzi, sijawahi kuwa Mwanachama wa chama chochote kile cha siasa zaidi ya CCM na sijawa na fikra za kubadili chama, natangaza nia ya kugombea Urais kupitia chama changu cha CCM, hii ya kwamba sasa hivi ni mapema mno kutangaza nia kwa sababu vyama havijafungua milango ya watu kutangaza nia, sio kweli…. watu wameweka nia za kuutaka Urais toka mwaka 1995 lakini pia kuweka nia sio kufanya kampeni, kinachokatazwa ni kuanza kufanya kampeni kabla ya muda wa kampeni kutangazwa’ –Dr. Hamisi Kigwangalla
‘Nimeamua kuweka wazi nia yangu, sitaki ule unafiki wa kujificha chini ya kivuli cha Ooooh!!….. nimeshauriwa, nimeombwa, nasubiri kuota, mimi ni mkweli na nimetia nia ya dhati kwamba nataka Urais’ –Dr. Kigwangalla
h15‘Vipaumbele vyangu kama napata fursa ya kuwa Rais ni kuboresha huduma za jamii kama maji, afya, elimu… kipaumbele cha pili ni kujenga na kuimarisha miundombinu kama barabara, ndege, reli na bandari…….. kipaumbele cha tatu ni utawala bora, nchi haiwezi kuongozwa bila kuwa na utawala wa sheria yani kila mtu apate haki yake bila kudhulumiwa ‘ –Dr. Kigwangalla

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni