Kurasa

Jumatano, 13 Agosti 2014

UMAKINI UNAHITAJI KUONGEZWA SERIKALINI

SERIKALI IJIPANGE KUZUIA MATUKIO YANAYOHATARISHA AMANI
Na Deonidas Mukebezi(UDSM)
Inakuwa haiingii akilini pale ambapo Serikali imekuwa ikihubiri kuwa Tanzania ni nchi ya amani ndani nan je ya nchi wakati kuna matukio yanayoashiria waziwazi kuwa amani inayohubiliwa kila siku na Serikali katika vyombo mbalimbali vya habari haipo kama inavyosemwa.
Katika nchi hii tumekuwa tukishuhudia mfululizo wa matukio mbalimbali ya kusikitisha na ambayo si ya kiubinadamu kama yale ya kuwaua vikongwe kwa tuhuma kuwa ni wachawi,mauaji ya walemavu wa ngozi ambao viungo vyao vimekuwa vikitumiwa kwa imani za kishirikina pamoja na mauwaji au uteswaji wa waandishi wa habari,matukio ambayo yamekuwa yakiibuka na kuondoka kama mitindo ya fasheni za nguo .
Pamoja na matukio yote hayo katikati ya mwezi wasaba mwaka huu yameibuka matukio mengine ya wizi wa watoto ambao haijulikani wahusika wanawaiba kwa minajiri gani ingawa wizi huo umekuwa ukienda sambamba na vitendo vya watoto kufanyiwa vitendo vya kikatili.
Mfano wa watoto ambao wameshapotea mpaka sasa ni pamoja na mtoto Merryn Reppyson ambae aliibwa na mtu asiefahamika eneo la Changanyikeni karibu nachuo kikuu cha Dar es salaam jijini Dar es salaam julai 15 na ambae mpaka sasa hajapatikana.
Jambo la kusikitisha ni kwamba wakati polisi wanasema wanafuatilia tukio moja,tukio jingine la aina hiyohiyo linaibuka.
Jambo hili linaumiza sana hususani wazazi wa watoto,lakini pia jamii ambayo sasa imekuwa ikiishi kwa hofu kuwa pengine watoto wao pia wanaweza kuingia katika kadhia hiyo.
Ni wazi kuwa jamii imechoshwa na matukio haya nan i jukumu la serikali kuwa na mipango endelevu ya kuhakikisha kuwa hayaibuki matukio ya ajabu ajabu ambayo yanaonekana dhahiri shahiri kuitikisa amani ya taifa letu ambayo imekuwa ikihubiliwa kila leo.
Pia serikkali inapaswa kutafuta na kutoa majibu sahihi pale ambapo wananchi walioipa dhamana kukaa madarakani wanapouliza maswali yanayotaka majibu ya haraka badara ya kubweteka na kufanya kazi kwa mazoea kwani wakati hausuburi na ya jana sio ya leo wala ya leo sio ya kesho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni