Kurasa

Jumanne, 22 Julai 2014

WATU NANE MASHAKANI SAKATA LA VIUNGO VYA BINADAMU


Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu wanane wanaoshukiwa kuhusika na sakata la kutupwa kwa mifuko zaidi ya 85 iliyokuwa na mabaki ya viungo mbalimbali vya binadamu kama vile vichwa,miguu,mikono,mioyo mapafu,vifua na mifupa mbalimbali iliyogundulika katika eneo la mbweni mpiji jijini Dar es salaam hapo tar 21/7/2014.

Watu hao ambao ni pamoja na madaktari wa hospitali ambayo pia ni chuo cha udaktari IMTU kilichopo jijini Dar es salaam wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya uchunguzi wa awali ambao umebaini kuwa mifuko hiyo ilitoka katika hospitali hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari,kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema kuwa viungo hivyo havikuwa na uvundo wala harufu yoyote na vilionekana kuwa vimekaushwa na kukakamaa.Kova alisema pia kuwa katika eneo hilo vilionekana vifaa vinavyotumika hospitari kama vile mipira ya kuvaa mikononi(gloves) nguo maalum(apron) na mifuko miwili iliyotunika pamoja na karatasi mbili zenye maswali na majibu.

"Viungo hivyo vilichukuliwa na kupelekwa muhimbili kwa uchunguzi zaidi na jopo la wapelelezi wakiongozwa na mkuu wa upelelezi kanda maalum ACP Japhar Mohamed walianza upelelezi mala moja kwakushirikiana na daktari wa jeshi la polisi anayehusika na uchunguzi wa miili ya binadamu(forensic Doctor) ambaye alishilikiana na madaktari wengine kutoka hospitali ya taifa Muhimbili"Alisema Kova

Kamanda Kova aliongeza kuwa baada ya uchunguzi ilibainika kuwa viungo hivyo kwa mala ya mwisho vilikuwa katika maabara ya chuo kikuu cha madaktari IMTU ambacho pia hufanya mafunzo ya udaktari kwa vitendo.

Kamanda Kova alisema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea na jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote ambae atagundulika kuhusika na tukio hilo na kuwataka wananchi watulie wakati polisi ikiendelea na uchunguzi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni