Kurasa

Jumamosi, 5 Julai 2014

AMTUPA MTOTO KWENYE KICHAKA KINACHOWAKA MOTO NA KUMSABABISHIA KIFO

Kigoma.Mkazi wa Kijiji cha Muhunga kilichopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma (Gloria Rubeben(20) anashikiliwa na polisi mkoani humo kwa kumtupa mtoto wake wa siku nne katika kichaka na hatimaye kufa baada ya kuungua na moto uliowaka katika kichaka hicho.
Akithibisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Frasser Kashai alisema Julai 2, 2014 majira ya saa 3.00 usiku katika kijiji cha Muhunga wilayani Kasulu Rubeben alifanya ukatili huo kwa mtoto wake , ambapo majirani waligundua kitendo hicho na kutoa tarifa sehemu husika.
Kamanda Kashai alisema , uchunguzi bado unaendelea ili kujua kiini cha mama huyo kufanya tukio hilo.
Katika tukio lingine Mwanamke mmoja, mkazi wa kijiji cha Minyima wilayani Kibondo atafikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kigoma kujibu tuhuma za kumuua mumewe.
Alisema Julai 2, 2014 saa 2.00 usiku mwanamke huyo alimpiga mumewe na figa la jikoni baada ya mumewe kuhoji ujio wa wageni watatu waliokuwa wamefika nyumbani kwake.Hata hivyo, KamandaKashai aliwaomba wanancchi wazidi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
MWANANCHI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni