Kurasa

Jumatano, 18 Juni 2014

VITA YA DR.NDUMBARO NA WAMBURA KUENDELEA LEO

KAMATI ya Rufaa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inatarajiwa kukutana leo mchana kupitia rufaa ya mgombea wa nafasi ya urais wa klabu ya Simba, Michael Wambura, anayepinga kuenguliwa kwa mara ya pili.
Wambura aliwasilisha rufaa kwa mara ya pili jana, baada ya Jumatatu iliyopita Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya Mwenyekiti wake Dk. Damas Ndumbaro kumuengua kwa madai ya kufanya kampeni kabla ya muda.
Akizungumza naTanzaniaDaimajana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Julius Lugaziya, alisema kamati yake itakaa leo saa 8 mchana kupitia rufaa hiyo.
Uchaguzi wa Simba unatarajia kufanyika Juni 29 kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, ingawaje hivi karibuni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilitangaza kuusitisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni