Kurasa

Ijumaa, 6 Juni 2014

RIBERY NJE KOMBE LA DUNIA

Mkufunzi wa Ufaransa amedhibitisha kuwa mshambulizi Frank Ribery hatashiriki kombe la dunia kutokana na jeraha.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 na anayechezea klabu ya Bayern Munich alijeruhiwa mgongoni wakati wa mazoezi siku ya Ijumaa.
“Ilimbidi kuwacha kufanya mazoezi kwa kuwa alikuwa akihisi uchungu mwingi sana,” Deschamps aliwaambia wanahabari baadaye.
‘’Hataweza kufanya mazoezi wala kucheza kwa majuma kadhaa.”
Ribery amejeruhi mgongo mazoezini
Lyon's Clement Grenier pia atakosa mashindano hayo kwa jeraha la nyonga.
Kiungo cha kati wa Southampton Morgan Schneiderlin na mshambulizi wa Montpellier Remy Cabella wamejumuishwa kikosini ili kucheza kwa niaba ya wawili hao.
Ribery alipelekwa kupigwa picha ya MRI, ambayo ilidhibitisha kiwango cha jeraha hilo.
Riberi alichaguliwa kuwa mchezaji wa tatu bora zaidi duniani mwaka wa 2013 nyuma ya mshindi wa Ballon d’Or Christiano Ronaldo wa Real Madrid na mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi.
BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni