Kurasa

Jumanne, 3 Juni 2014

MASKINI KITOTO NASRA:BENDERA ALIA MSIBANI,ASEMA WAZAZI NA NDUGU WALAANIWE KUANZIA DUNIANI MPAKA MBINGUNI

WAKATI mamia ya wakazi wa mji wa Mororgoro wakijitokeza kwa wingi kumzika mtoto Nasra Rashid (4) aliyefichwa katika boksi tangu akiwa na miezi mitatu, viongozi wa dini na serikali wamelaani kitendo cha ukatili alichofanyiwa na wazazi wake.
Mtoto huyo alizikwa jana mkoani hapa baada ya wananchi wengi kujitokeza kutoa salamu zao za mwisho katika Uwanja wa Jamhuri.
Katika salamu zake za rambirambi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, aliiomba mahakama na Jeshi la Polisi mkoani hapa kutokuwa na huruma na wazazi hao.
“Bila kutafuna maneno, huruma wala haya kwa yeyote hapa, ukatili huu uliomfungulia pepo mtoto huyu baada ya kufanyiwa mateso, dhambi hii iwatafune kuanzia sasa hapa hapa duniani na hata baadaye mbinguni,” alisema Bendera akionyesha kububujikwa machozi.
Alisema haiingii akilini kwa mtoto mwenye baba, mama, ndugu na jamaa wachamungu, wakamficha na kumtesa kwenye boksi kwa zaidi ya miaka mitatu kwa sababu ya aina yoyote iliyopo hapa duniani halafu aliyetenda unyama huo akafurahiwa.
“Jamani tumuogope na kumtii Mungu, haifurahishi wala haifai kusimulia, nawaomba mahakama mkishirikiana na polisi mpeleleze hawa ambao hata dhamana wamekosa, wateseke kama alivyoteseka mtoto Nasra,” aliongeza.
Alisema tafakari zake zimebaini kuwa unyanyasaji kama huo kwa watoto, walemavu na jinsia kwa jamii unaota mizizi na kukua nchini kutokana na wananchi kuacha mila na desturi za ujamaa na usalama kwa kutotembeleana na kujuliana hali.
Bendera alimgeukia baba wa marehemu, Rashid Mvungi na kumwambia bayana kuwa ana laana ya kufa na haikwepi kwa mateso aliyopata mtoto wake.
“Ndugu yangu Mvungi bila hata kukuonea haya, una laana ya kufa, hii hukwepi na adhabu yako ipo kuanzia hapa duniani,” alimweleza mzazi huyo aliyehudhuria mazishi hayo.
Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulazizi Abood, alisema msiba wa Nasra umekuwa gumzo katika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma na kuamsha fedheha nyingine kwa taifa ukiuonyesha mkoa kutokuwa na huruma kwa watoto.
“Kama kuna wengine wanafanya hivi, basi nawasihi waache na kama hawawataki watoto hao wawalete tuwatafutie watu wa kuwalea, nina imani wapo wanatafuta watoto,” alisema.
Akihitimisha maombolezo uwanjani hapo, Sheikh wa Mkoa wa Morogoro, Ally Omari, alisema mateso ya mtoto huyo hayawezi kutenganishwa na ushirikina kwa kuwa wazazi na walezi walilifahamu jambo hilo na kuendelea na shughuli zao.
Akionyesha kukerwa na mtoto huyo kufanywa ‘ndondocha’, Sheikh Omari alisema wazazi wa sasa wakiwemo wa Nasra wanaendekeza ‘michepuko’ ambayo mwisho wake ni aibu kama iliyojitokeza.
Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungantitu, alisema taasisi hiyo imekuwa si kimbilio kwa wenye matatizo kutokana na kutokuwa na ofisi.
Mwili wa marehemu Nasra ulizikwa kwenye makaburi ya Kola mjini hapa kwa taratibu za
TANZANIA DAIMA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni