Kurasa

Jumamosi, 10 Mei 2014

PINDA AMKIMBIZA OFISINI MEYA WA BUKOBA.

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amefuta ndoto za aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk. Anatory Amani akisema kuwa, Serikali inatambua kuwa alijiuzulu tangu Januari mwaka huu, ilipowasilishwa ripoti ya Mdhibiti na Mkakaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Ludovick Uttouh.
Pinda alisema kuwa suala hilo lilikwishamalizika na kwamba ameshangazwa na hatua ya Dk. Amani kugeuka kauli yake na hivyo kuibua tena mgogoro.
Pinda alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akihitimisha hoja za wabunge waliochangia hotuba ya wizara yake, hususan mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki (CCM), aliyedai ofisi ya Waziri Mku imeshindwa kumchukulia hatua Dk. Amani.
“Hili suala la manispaa ya Bukoba lilikwisha malizika na Dk. Amani sio meya tena. Kwa taarifa nilizopewa na naibu wangu aliyeniwakilisha wakati ripoti ya CAG ikisomwa mbele ya Baraza la Madiwani na mkuu wa mkoa, na nilitazama video ya kikao kile, huyu alijiuzulu.
“Alitii uamuzi tuliyompa pamoja na watuhumiwa wote waliotajwa katika ripoti ile kuhusika na ubadhilifu. Sasa kuhusu baadhi ya madiwani kufungua kesi ya kuzuia baraza lisikutane, mimi nawasihi wawaonee huruma wananchi na kuifuta,”alisema.
Pinda aliongeza kuwa ofisi yake kupitia wanasheria, inafanya utaratibu wa kushauriana na mahakama ili kuondoa kesi iliyopo na hivyo kuruhusu madiwani kuendelea na vikao vyao kama kawaida.
Akichangia hotuba hiyo juzi, Kagasheki alisema wananchi wa manispaa ya Bukoba wako msibani kutokana na ofisi ya waziri mkuu hatowajali kumaliza mgogoro huo uliyodumu tangu Aprili 2012 hadi Mei 2014.
Januari 16 mwaka huu, Uttouh aliwasilisha ripoti yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyokuwa ikitekelezwa na Dk. Amani, akaisema kuwa utekelezaji wake ulifanyika kifisadi bila kuzingatia idhini ya Bazara wala wizara husika.
Tanzania Daima lilikuwa la kwanza kukifichua ufisadi huo na kuuripoti mfulilizo tangu Mei, 2012, hadi Dk. Amani alipotiwa hatiana na kujiuzulu, huku mkurugenzi wake, Hamis Kaputa, mhandisi, Steven Nzihirwa na mhasibu wa halmashuri, Hamdun Ulomy wakivuliwa madaraka yao.
CAG katika ripoti yake kuhusu uwekezaji wenye mashaka kwenye kituo cha kuosha magari, alisema zabuni haikuwa shindanishi na kwamba ilikuwa kinyume cha taratibu.
Alisema kuwa waliosaini ni mkataba huo ni Khamis Kaputa aliyekuwa mkurugenzi kabla ya kuhamishiwa mkoani Mbeya na meya Amani huku wakijua ilikuwa ni makosa kufanya hivyo bila idhini ya kikao cha madiwani.
Uttouh alifafanua kuwa Kamupuni husika ya ASEC iliyofanya kazi hiyo haijasajiliwa na Msajili wa makambuni (Brela) na hailipi kodi TRA.
Kuhusu tuhuma za upimaji na ugawaji wa viwanja, ripoti ilibaini kuwa kati ya wananchi 800 waliotakiwa kugawiwa viwanja ni wananchi 300 ndio waliogawawia kutokana na migogoro ya viwanja kimila.
“Manispaa ilingia makubaliano na Mfuko wa Damana ya Uwekezaji (UTT) kupima viwanja 5000 kwa kugawana faida ya asilimia 50 kwa 50 na UTT.
“Mkataba huo ulisainiwa na Kaimu meya, Ngalinda, kwa upande wa manispaa bila kupata idhini ya Baraza la Madiwani na mkopo huo ulichukuliwa bila bila kupata ridhaa ya waziri mwenye dhamana,”alisema.
Alisema kuwa mradi huo garama za faida zilikuwa zinabadilika kila mara na walikusudia kupata sh. bilioni 1.2 lakini ziliongezeka hadi kufikia sh. bilioni 4.8 na zilizoonekana kwa CAG ni sh. bilioni 4.6, kwa hiyo milioni 200 hazijulikani zilipo.
Uttouh aliongeza kuwa kuhusu tuhuma za matengenezo ya barabara mpya, manispaa ya Bukoba iliingia mkataba na mkandarasi aitwaye Kajuna Investment wa sh.milioni 138.
Alisema kuwa mkandarasi huyo alilipwa fedha za dharula ambazo hazikuwa na nyaraka, hivyo malipo hayo yaliongezwa hadi kufikia sh. milioni 227 kwa kutumia barua iliyosainwa tofauti na ili ya awali.
“Malipo hayo hayakuwa na idhini ya mkandarsi wa serikali na yalikuwa kinyume na kanuni za manunuzi ya umma,”alisema.
Uttouh katika tuhuma za mradi wa ujenzi wa soko kuu la mjini Bukoba, alisema kuwa walibaini kuwa utaratibu haukupata idhini ya madiwani ya kumlipa mkandarasi mshauri OGM Consultant sh.milioni 789.
Kwamba meya Amani pia aliwaita madiwani na kuwaeleza kuwa mkandarasi anahitaji jumla la sh. miliini 590, jambo ambalo mmoja wa madiwani wa kata ya Kitendagulo, Samwel Ruhangisa alikataa pale pale kwenye kikao.
CAG aliagiza kuwa kampuni hiyo ya OGM irudishe sh. milioni 33 zilizotumika kinyume na mkataba.
“Sh. milioni 200 zilizotumika kumpata OGM Consultant ya Dar es Salaam hazikufuata utaratibu kutolewa na mkataba mwingine uliosainiwa kinyume cha sheria na OGM ni sh. milioni 700 ambapo madiwani waliambiwa ni milioni 400 na kampuni hiyo hailipi kodi TRA.
Kwa mujibu wa Uttouh, OGM hakuwa kwenye orodha ya walioomba zabuni ya kufanya kazi ya ukandarasi ushauri katika ujenzi wa soko kuu lakini alionekana kwenye orodha baadye ya waliolipwa.
“Wakandarasi wote waliolipwa fedha hizo walikuwa hawalipi kodi TRA, hivyo mamlaka hiyo ina haki ya kuwadai hizo kodi,” alisema.
Kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi Bukoba, CAG alisema mradi huu hakutangazwa kwenye gazeti la sertikali lakini walipata mkandarasi na kumlipa fedha za kazi hiyo kinyume na taratibu za serikali.
“Gazeti lilotangaza tenda hiyo halikupatikana, pia timu ya ukaguzi ilitembelea eneo la kazi na kubaini kuwa mkandarasi alilipwa fedha nyingi tofauti na kazi aliyoifanya,”alisema.
VIA TANZANIA DAIMA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni