Kurasa

Alhamisi, 15 Mei 2014

MLINZI Bakari Mape (70) mkazi wa Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani ameuwawa kwa kunyongwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Watu hao ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja walimwua mlinzi huyo kwa kumvunja shingo kisha kuiba kwenye duka ambalo mlinzi huyo alikuwa akililinda.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Mwandamizi Msaidizi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 14 mwaka huu majira ya saa 8 usiku eneo la sokoni Mlandizi wilayani hapa.
Kamanda Matei alisema kuwa watu hao baada ya kumwua marehemu ambaye alikuwa akilinda duka la Conrad Masawe (53) mkazi wa Mtongani Mlandizi, waliiba kiasi cha shilingi milioni 5.2.
"Walipomwua walingoa bati kisha kuingia ndani na kuiba fedha hizo na kutoweka kusikofahamika huku wakimwacha marehemu hapo," alisema Kamanda Matei.
Alisema kuwa kutokana na tukio hilo wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Omary Rajabu kuhusiana na suala hilo.
"Mwili wa marehemu ulikabidhiw andugu kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa daktari na tutawasaka watu walihusika na tukio hilo ili mkondo wa sheria uweze kuchukua hatua kwani kitendo hicho ni ukatili ndani ya jamii," alisema Kamanda Matei.
Aidha aliwataka wafanyabiashara waajiri watu weny umri wa kati ili waweze kukabiliana na matukio kama hayo na kuacha kuajiri watu wenye umri mkubwa sana kwani ni vigumu kukabiliana na matukio kama hayo.
Via:Michuzi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni