Kurasa

Jumanne, 13 Mei 2014

JOKATE ATOA SOMO KWA WANAFUNZI UDSM.


Mshindi wa pili wa miss Tanzania 2006 Jokate Mwegelo aka Kidoti amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu kuachana na mawazo ya kuajiliwa mala baada ya kuhitimu masomo yao.
Akizungumza katika kongamano lililofanyika katika ukumbi wa Nkuruma chuo kikuu Dar es salaam miss huyo ambae kwasasa anamiliki kampuni yake inayohusiana na mitindo ya nguo na nywele,alisema kuwa tatizo linalowakabili wanafunzi wengi ni kuwa na mawazo ya kuajiliwa mala baada ya kumaliza masomo yao na inapotokea kuwa hawakuajiliwa basi wanahisi kama ndio mwisho wa maisha.

Jokate alizungumza hayo akitolea mfano wa yeye mwenyewe ambapo alisoma masomo ya siasa ambayo mpaka sasa hajaifanyia kazi elimu yake kitu chochote zaidi ya kufuata vipaji vyake.
Jokate alisema soko ni gumu lakini anaendelea kupambana mpaka afikie malengo yake ya kuwa milionea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni