Kurasa

Jumatatu, 19 Mei 2014

HII NDIO CV YA KOCHA MPYA WA MANCHESTER UNITED KWA KIFUPI

Hatimaye Manchester United wamemtangaza rasmi Louis Van Gaal kuwa kocha wao kuanzia msimu ujao.
Louis Van Gaal ambaye alizaliwa miaka 62 iliyopita nchini Uholanzi anakuwa kocha wa kwanza kabisa kutoka nje ya Uingereza na visiwa vyake kuifundisha klabu ya Manchester United.
Van Gaal amewahi kuvichezea vilabu vya Ajax, Royal Antwerp, Telstar, Sparta Rotterdam, AZ Alkmaar, pia amewahi kuvifundisha vilabu vya Ajax ambapo alishinda vikombe vitatu vya ligi kuu, vikombe vitatu vya michuano ya Johanny Cruyff, kombe moja la Champions League, UEFA Cup mara 1, na kombe la mabara vilabu mara 1.
Akatoka Ajax na kuhamia FC Barcelona ambapo alichangia sana kuwainua makinda akina Lionel Messi, Xavi Hernandez na Andres Iniesta pamoja na kipa Victor Valdes – aliwawezesha kushinda La Liga mara 2, UEFA SuperCup 1, Copa 1.
TZA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni