Kurasa

Jumatatu, 19 Mei 2014

GIGGS ASTAAFU SOKA.

Muda mchache baada ya kutangazwa kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Manchester United, mwanasoka Ryan Giggs ametangaza rasmi kustaafu soka.
Giggs ambaye alianza kuichezea timu ya watoto ya Manchester United mnamo mwaka 1991, amestaafu soka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 23 mpaka sasa huku akifanikiwa kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika klabu yake ya Manchester United – akiichezea mara 963.
Giggs anastaafu akiwa ndio mwanasoka ambaye kashinda makombe mengi zaidi – makombe 13 ya premier league, FA Cup 4, Capital One 4, mawili ya kombe la klabu bingwa ya ulaya na 2 klabu bingwa ya dunia.
Giggs pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa ligi mara mbili mwaka 1992 na 1993, pia alishinda tuzo hiyo kutoka kwa klabu ya Manchester United mwaka 1991 na 1992.
Mnamo mwaka 2009 alishinda tuzo ya BBC Sports Personality of the Year na paia akashinda PFA Player of the Year award. Ametajwa kuwa mchezaji bora mwaka wa ligi kwa mara 6.
TZA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni