Kurasa

Ijumaa, 9 Mei 2014

DAWA YA UZEE YAPATIKANA

Watu wengi wangetamani kuona hawazeeki, wanabakia na nguvu za ujana na kwa sababu hiyo wanasayansi wanatafiti kupata ufumbuzi.
Vyuo vikuu vitatu maarufu duniani vimekuja na matokeo ya utafiti ambao unaweza kukata kiu ya wengi ambao hawatamani kamwe kuzeeka.
Siku hizi kumekuwapo na usemi kuwa uzee mwisho Chalinze, jijini (Dar es Salaam) kila mtu ‘baby’ (mtoto). Hii ikiashiria watu hawapendwi kuitwa wazee ingawa umri wao ni mkubwa.
Wamekuwa na kauli hiyo ili kulazimisha mazingira kwamba bado wana uwezo wa kufanya yote kama wenye damu changa lakini katika uhalisia si kweli.
Utafiti wa vyuo vya Harvard na California vya nchini Marekani vikishirikiana na Cambridge nchini Uingereza, unajenga mazingira ya kuifanya ndoto ya wenye mawazo ya kuukataa uzee kuwa kweli.
Watafiti hao walichukua damu ya panya mchanga na kumuingizia kwa aliyezeeka. Walichobaini ni kwamba panya yule mzee alichangamka na kurejewa na nguvu za ujana.
Matokeo ya utafiti huo yanatoa mwanya kwa wanasayansi kukaa kitako na kutengeneza dawa ambayo mtu akitumia anaweza kutozeeka.
Kutozeeka huko ni kuendelea kuwa na dalili za ujana kama vile kutokuwa na makunyanzi usoni na viungo kuendelea kuwa na nguvu ya kutekeleza mambo yote kama kawaida hata wenye umri wa zaidi ya miaka 70.
Utafiti ulivyofanyika
Timu ya watafiti hao wiki hii walitangaza kuwa wamegundua namna ambayo wanaweza kumfanya panya mzee kutokuwa na dalili zinazofanana na umri huo.
Wanasema kwenye utafiti huo kuwa mara baada ya kuchukua damu ya panya mchanga na kumuingizia aliyezeeka ghafla alibadilika na kurejewa na nguvu zilizomfanya achangamke na kutenda kama vile bado hajazeeka.
Walichobaini ni kwamba ile damu ilienda kuchangamsha ubongo kiutendaji na kuwezesha kuimarika kwa utendaji wa mwili kwa jumla.Kwa kawaida mambo yote yanayotendeka mwilini huongozwa na ubongo kwa kuhamasisha homoni fulani kulingana na jambo husika.
KUTOKA MWANANNCHI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni