Kurasa

Jumamosi, 19 Aprili 2014

SIMBA NA YANGA HII NAYO INAKUJA!ISUBIRINI.

Dar es Salaam. Uongozi wa timu ya soka ya Ndanda FC ya Mtwara umepanga kusaka Sh900 milioni kwa ajili ya kufanikisha ushiriki wa timu hiyo katika Ligi Kuu msimu ujao.
Katibu Mkuu wa Ndanda FC, Suleiman Kachele alisema lengo ni kuhakikisha timu hiyo inaonyesha ushindani wa kweli katika Ligi Kuu msimu ujao badala ya kuwa mshiriki pekee.
Kachele alisema kuwa fedha hizo zitakusanywa kupitia wadhamini mbalimbali na wadau wa soka wa Mkoa wa Mtwara.
“Tunataka udhamini wa Vodacom na Azam uchangie tu, lakini bajeti halisi ni Sh900 milioni ambayo itatosheleza timu yetu iweze kushindana na si kushiriki.
“Tutatafuta wadhamini tofauti kwa ajili ya kufanikisha dhamira yetu hiyo,” alisema Kachele

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni