Kurasa

Ijumaa, 18 Aprili 2014

POMBE SIGARA NA CHUMVI CHANZO CHA SARATANI YA UTUMBO


Kila siku magonjwa yanazidi kuibuka duniani na kusababisha hofu . Hata hivyo maradhi mengi huchochewa na mfumo wetu wa maisha, kama aina za vyakula na starehe.
Maradhi ya saratani yameendelea kushika kasi duniani kote na kusababisha taharuki kwa watu maskini na hata matajiri. Saratani huweza kuathiri sehemu yeyote ya mwili wa binadamu.
Kwa mfano, saratani huweza kujitokeza katika utumbo wa chakula. Eneo muhimu ambalo hakuna awezaye kukwepa kulitumia na visababishi vyake vinatajwa kuwa ni mamboe tuyafanyayo kila mara katika maisha yetu.
Iko mifano mingi kama vile utumiaji wa chumvi nyingi, uvutaji wa sigara, vyakula vilivyokaushwa kwa moshi (samaki, nyama), pombe na kemikali.
Saratani ya utumbo wa chakula ni saratani ambayo hutokea katika katika kifuko cha misuli midogomidogo iliyopo kati ya eneo la juu ya tumbo na mbavu.
Eneo ambalo hupokea chakula na kusaidia kupokea na kukipeleka katika makutano ambayo husagwa na majimaji yake kuingia mwilini kwa ajili ya kusaidia mfumo mzima wa uendeshaji wa mwili.
Kwa mujibu wa watafiti wa saratani wa nchini Marekani, saratani hii haitakiwi kufananishwa na saratani nyingine ya tumbo kama vile ya ini, kongosho, utumbo mkubwa na mdogo, kwa sababu kila moja ina dalili na sababu zake.
Sababu za saratani ya utumbo
Daktari Ally Mzige, wa kliniki ya AAM, inayoshughulika na afya ya uzazi, vijana, wanawake na watoto, anazitaja sababu za saratani ya utumbo wa chakula kuwa ni pamoja na kuwa na umri mkubwa. Anasema watu wengine hupata ugonjwa huo wakiwa na umri wa miaka 55 hadi 95, lakini wengi wakiwa katika umri wa kuanzia miaka 90 na kuendelea.
Pombe na sigara
Anaitaja sababu nyingine kuwa ni matumizi ya pombe na sigara, ambayo yanatajwa kuwa ni chanzo cha saratani ya karibu aina zote. Hata hivyo, sigara huongoza kwa kusababisha saratani ya utumbo kwa kuwa unapovuta moshi na kutoa nje unameza baadhi ya kemikali bila kukusudia. Sigara inasababisha saratani ya utumbo wa chakula kwa wastani wa mtu mmoja hadi watano sawa na asilimia 20,” anasema Mzige.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni