Kurasa

Ijumaa, 18 Aprili 2014

MANZANIA WA KWANZA ACCOUNT YAKE YA FACEBOOK KUTHIBITISHWA.

Flaviana Matata amekua mwakilishi mzuri wa Tanzania kwenye nchi mbalimbali alizofanya kazi kama Ufaransa, Hispania na Marekani ambako anaishi sasa hivi New York.
Flaviana amethibitishwa rasmi na facebook kwamba hiyo account yenye hicho kitiki hapo juu ndio account yake pekee na halali hivyo ule utapeli ambao ulikua unafanywa kwa kutumia account nyingine feki za Flaviana utaishia hapa.
Flavvy anakua Mtanzania wa kwanza ninaemfahamu kuwa verified na facebook ambapo tayari kwenye account yake ya twitter yuko verified pia ambapo Watanzania wengine ambao wako verified twitter ni President Jakaya, Hasheem, Ay, mawaziri January Makamba na Lazaro Nyalandu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni