Kurasa

Ijumaa, 18 Aprili 2014

KUMBE MIMEA PIA HUPENDA MUZIKI!SOMA HAPA.

Hivi unajua kwamba mimea ina hisia? Unajua pia inasikia maumivu?
Mwanafizikia aliyebobea katika sayansi ya mimea kutoka nchini India, Jagadis Chandra Bose alitumia kipindi kirefu katika maisha yake kutafiti na kujifunza kwa vitendo namna mazingira ya mimea na kuthibitisha kwamba inaguswa na baadhi ya tabia za viumbehai.
Pia alithibitisha kwamba mimea ni kama binadamu, kwani inahisi na inaguswa na mazingira ya nje kama vile mwanga, baridi, joto na kelele au sauti.
Maelezo hayo yamechapishwa ili kutunza kumbukumbu katika vitabu vyake vyaResponse in The LivingnaNon-Livingvilivyochapishwa mwaka 1902 naThe Nervous Mechanism of Plantskilichochapishwa mwaka 1926.
Mwanasaikolojia Modesta Kimonga, kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma anakubaliana na utafiti huo kwamba mimea ina tabia zinazolandana na binadamu au viumbehai kwani hutegemeana.
“Mimea ni viumbehai kama ilivyo kwa binadamu. Mimea hutoa hewa ya oksijeni wakati wa mchana na binadamu hutoa hewa chafu (carbondioxide). Hata hivyo inaweza kuwa na tabia za kibinadamu kwani huwa na mapokeo chanya na wakati mwingine huonyesha mijibizo ikiwa itahamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kama ilivyo kwa binadamu,” anasema Kimonga.
Anafafanua kuwa licha ya mimea na binadamu kuwa na mapokeo sawa, wakati mwingine hawafai kuwa pamoja “ndiyo maana hutolewa ushauri kwamba mimea haipaswi kulala ndani wakati wa usiku, kukiwa na binadamu”.
Kimonga anasema muziki ni sehemu ya faraja kwa kiumbehai hivyo mimea hupata mitetemo ya sauti yenye ladha ya muziki.
“Hii ipo kwa wanasayansi waliofanya tafiti miaka kadhaa nyuma, lakini si mimea inayoishi karibu na binadamu tu. Ukiwa porini kuna sauti nzuri za ndege wa aina mbalimbali usiku na mchana, husaidia mimea kukua kwa uharaka zaidi. Kuna sauti zitokanazo na upepo unaopuliza kwenye miti mirefu hutoa mitetemo ya sauti pia,” anasema.
Anasema mimea ni kama binadamu, ndiyo maana binadamu asiyependa muziki mara nyingi huwa na matatizo, kwani hukosa kufarijiwa na muziki.
Mimea huzungumza
Mtaalamu mwingine wa mimea kutoka Marekani, Luther Burbank aligundua namna ambavyo mimea inaweza inaweza kuonyesha ishara tofauti iwapo utahamishwa kutoka sehemu ulipooteshwa na kupelekwa sehemu nyingine ambayo haina sauti au ina sauti.
KUTOKA MWANANCHI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni