Kurasa

Ijumaa, 18 Aprili 2014

JESHI LA KUIUA SIMBA HILI HAPA.

Kikosi cha Young Africans
Young Africans imerejea jana jijini Dar es salaam na kuendelea na maandalizi ya mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya timu ya Simba SC mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa siku ya jumamosi majira ya saa 10:00 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Kikosi cha Young Africans kimeweka kambi eneo la Bahari Beach kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kwa watoto wa Jangwani kuhakikisha wanafanya vizuri na kupata ushindi mzuri wa kumalizia ligi.
Kocha Mkuu wa Young Africans amesema vijana wake wapo katika hali nzuri kuelekea mchezo wa jumamosi, kwani hakuna majeruhi hata mmoja katika kikosi chake cha wachezaji 20 walioingia kambini kujiandaa na mchezo huo.
Hans amesema Vijana wake wanazidi kuonyesha mabadiliko makubwa kiuchezaji, mafunzo yake wanaonekana kuyaelewa vizuri hivyo kikubwa anaomba waendelee kuwa katika hali nzuri kuelekea mchezo na ana imani kikosi chake kitaibuka na ushindi.
"Nina uzoefu na michezo wa watani wa jadi, huwa inakua migumu kwa kila timu kutokana na kila timu kutaka kuonyesha wapenzi, washabiki na wanachama wake kuwa wako vizuri, Simba ni timu nzuri lakini bado sioni kikwazo cha kutuzuia tusiibuke na ushindi katika mchezo huo" alisema Hans.
Leo jioni kikosi kitafanya mazoezi katika Uwanja wa Bko Beach Veterani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo wa jumamosi ambapo kikosi cha Young Africans mpaka sasa kinashika nafasi ya pili kikiwa na pointi 55 huku kikiwa kimecheza michezo 25, Simba wakiwa nafasi ya nne na pointi 37 huku wakiwa wamecheza michezo 25.
Kikosi cha Young Africans kilichoingia kambini kujiandaa na mchezo huo ni:
Walinda milango:Deogratias Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi:Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ibrahim Job, Rajab Zahir, Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo:Frank Domayo, Hassan Dilunga, Salum Telela, Hamis Thabit, na Nizar Khalfani
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Mrisho Ngasa, Jerson Tegete, Hamisi Kizza, Hussein Javu na Saimon Msuva.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni